Pages

Saturday, October 3, 2015

RONALDO AFANYIWA PARTY BAADA YA KUVUNJA REKODI YA MAGOLI BERNABEU


Ronaldo aliisaidia timu yake ya Real Madrid kuifunga Malmo katika Uwanja wa SwedBank nchini Sweden katika mechi ya Mabingwa Ulaya baada ya kufunga mabao mawili na kuvunja rekodi ya ufungaji magoli kwa klabu hiyo.
Acto Cristiano
Ronaldo amelingana na mfungaji mkongwe wa Real Madrid, Raul Gonzalenz kwa magoli 324 katika michuano yote huku pia akifikisha magoli 500 katika jumla ya magoli toka aanze kusakata kandanda.
Ronaldo sasa amefikisha magoli 501 ambayo yamepatikana katika klabu za Sporting Lisbom, Manchester United na Real Madrid aliojiunga nao katika majira ya joto ya mwaka 2009 akitokea Old Trafford.
Real Madrid iliamua kufanya sherehe maalumu ya kumpongeza Ronaldo ambapo alitumia nafasi hiyo kuwashukuru wachezaji wote ambao wam,empa ushirikiano hadi kufikia mafanikio hayo.
Klabu ya Manchester united ilimpongeza baada ya kuvunja rekodi hiyo kupoitia ukurasa wake wa Twitter wakimshukuru kwa magoli 118 aliyowafungia akiwa Old Tarfford.
Ronaldo amefikisha magoli 324 baada ya mechi 308 tu tofauti na mkongwe Raul aliyetumia mechi 741 kufikisha magoli hayo hayo katika klabu aliyoichezea ujana wake wote.
Acto Cristiano



No comments:

Post a Comment