Pages

Thursday, December 3, 2015

NEVILLE ATEULIWA KUIFUNDISHA VALENCIA

 


Beki wa zamani nguli wa klabu ya Manchester United, Garry Neville ameteuliwa kuiongoza timu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania, La Liga.
Maamuzi hayo yamekuja ghafla baada ya kocha aliekua akiifundisha timu hiyo Nuno Espirito Santo kuachia ngazi katikati ya msimu huku mechio ya kwanza ya Neville itakua dhidi ya Lyo, mechi ambayo lazima Valencia ishinde ili iweze kufuzu kwenda raundi ya mtoano ya Champions League.
Neville, 40 amemteua mdogo wake wa damu, Phil Neville kama kocha msaidizi baada ya Phili kujiunga na klabu hiyo katika benchi la ufundi mapema January mwaka huu.
Neville anakua mchezaji wa 29 kutoka katika utawala wa Ferguson kuwa kocha baada ya uteuzi huo. Sir Alex Ferguson alimpongeza Neville kwa uteuzi huo huku akimsifia kuwa ni kiongozi mzuri ndani na nje ya uwanja kwa hiyo itakua ni nafasi nzuri kwake kuonyesha ulimwengu wa soka kitu alichonacho kama kiongozi.
Naye Kocha wa timu ya Taifa ya England, Roy Hogson amempongeza Neville kwa hatua hiyo huku akisema kuwa nafasi ya Garyu katika timu ya taifa iko pale pale na haitaatiriwa na uteuzi huo. Garry amekua katika benchi8 la ufundi la England kwa muda sasa.
Wachezaji wengine waliofanikiwa kuwa wakufunzi kutoka katika kikosi cha Ferguson ni kama Viv Anderson, Michael Appleton, Henning Berg, Clayton Blackmore, Laurent Blanc, Steve Bruce, Chris Casper, Peter Davenport, Simon Davies, Darren Ferguson, Ryan Giggs, David Healy, Gabriel Heinze, Mark Hughes, Paul Ince, Andrei Kanchelskis, Roy Keane, Henrik Larsson, Gary Neville, Paul Parker, Mike Phelan, Bryan Robson, Mark Robins, Teddy Sheringham, Ole Gunnar Solskjaer, Frank Stapleton, Gordon Strachan, Chris Turner, Neil Webb.

No comments:

Post a Comment