Pages

Saturday, November 28, 2015

MPINZANI MKUU WA RAIS AMEKUWA WAZIRI MKUU

waziri mkuu(Kulia) Somji Rodgers akiapa mbele ya Makamu wa Rais  Steven Mjema
Bunge la Chuo Kikuu cha Tumaini limempitisha Somji Rodgers kuwa Waziri Mkuu kwa idadi ya kura 20 kati ya 21, ambapo aliyepinga uteuzi huo ni mbunge mmoja tu.
Rogers ambae alikuwa ni mshindani wa Rais Khalifa Rashid katika kinyang'anyiro cha kiti hicho hapo Julai mwaka huu na kuwa mshindi wa pili.
Rogers alichukua nafasi hiyo mara baada ya Waziri Mkuu wa kwanza mteule, Ayub Luhunga kutopitishwa  na Bunge hilo siku ya Alhamis ya Novemba 26,2015
"Nitajitahidi kushirikiana na rais wangu ili tuweze kutetea maslahi ya wanafunzi ambao wana imani kubwa nasi katika serikali hii" alisema Rogers.
Rogers alisema anamshukuru rais kwa kumteua kuwa Waziri Mkuu wake kwa kumuamini na kumpa majukumu mazito na aliahidi kuwa atayaweza japokuwa hapo mwanzo kila mmoja alikuwa na vipaombele vyake wakati wa kuwania kiti hicho na rais Rashid Khalifa.



No comments:

Post a Comment