Pages

Sunday, September 27, 2015

MESSI NJE MIEZI MIWiLI

Mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Leonel Messi atakua nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa kuanzia wiki saba hadi nane kufuatia majeraha aliyopata wakati timu yake ikiifunga Las Palmsa huku kuumia kwake kukiwasha taa ya hatari kwa mabingwa wa Ulaya na Hispania.
Barcelona walitarajia mengi kutoka kwa Messi aktika ,echi hiyo baada ya kipigo kutoka kwa Celta Vigo katikati ya wiki iliyopita lakini Messia laitunia dakika tisa tu kabala ya kutolewa nje kwa matibabu.
Messi atakosa mechi zaidi ya nane ana kuna uwezekano akakosa mechi ya Classico hapo November 21.
Kwenye Ligi ya Mbaingwa Ulaya Messi atakosa mechi dhidi ya Leverkusen na BATE Borisov nyumbani na ugenini lakini kukosekana kwa Messi kuna athari zaidi katika La Liga ambapo Barcelona wanahaha kuubakisha ubingwa nyumbani.
Messi atakosa mechi za Sevilla, Getafe, Rayo Vallecano, Eibar, Villarreal na kuna uwezekano akawa hajawa fiti kuivaa Real Madrid katika El Clasico ambayo itakuja baada ya wiki ya mechi za kimataifa November.
Kimataifa Messi anaweza kukosa mechi za kufuzu kombe la dunia dhidi ya Paraguay, Ecuador, Brazil na Colombia.
Kukosekana kwake kwenye mechi hiyo ya Real Madrid kunazua shaka ukilinganisha jinsi timu hizo zilivyoanza msimu huu huku Real ikiwa imara zaidi ya mabingwa hao wa La liga msimu uliopita.
Barcelona wa,ekua mashaka kwenye safu yao ya ulinzi inayolindwa na Pique na Mascherano baada ya kuruhusu magoli mengi na ya kizembe katika mechi za msimu huu huku Messi na Neymar kwa pamoja wakikosa penalty tatu kati ya nne walizopata msimu huu.

No comments:

Post a Comment