Beckham na Sir Alex Ferguson watakutana tena safari hii wakiwa viongozi wa timu ya World XI huku Ferguson akiwa kocha na Beckham kama kiongozi wa timu.
Mechi hiyo pia itahusisha mwamuzi wa zamani wa soka aliyepata heshima kubwa, Muitaliano Perluigi Collina huku Carlo Anceloti akiiongoza timu ya upande wa pili.
Zinedine Zidane atajumuishwa kwenye mechi hiyo ambayo hela zitakusanywa kupelekwa katika mfuko wa UNICEF ambao Beckham ni balozi wake.
Beckham alistaafu miaka mitatu iliyopita alisema hakutegemea tena kuvaa viatu vya soka lakini itakua siku nzuri kumuona Anceloti , Zidane na Ferguson tena.
Ferguson, 73, alistaafu mwaka 2013, akiwa ameshinda vikombe 38 katika miaka 26 aliyokaa pale Old Trafford.
No comments:
Post a Comment