Pages

Monday, June 29, 2015

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, HARRISON ATANGAZA NIA

Ukiwa mwaka wa uchaguzi mkuu ambapo wananchi watapata nafasi ya kuchagua viongozi kuanzia kwa Rais, wabunge na madiwani baadhi ya vijana wamejitokeza kutangaza nia katika nafasi mbalimbali zaki uongozi.

 HARRISON LUKOSI kutoka Chuo Cha Tumaini kitivo cha sheria amekuwa mmoja ya watangaza nia ya kugombea kiti cha udiwani katika kata ya msasani Jijini Dar es Salaam.
Harrison katika ubora wake
 LUKOSI ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa kwanza kitivo cha sheria amesema sababu za yeye kutangania ya kugombea kiti hicho ni kutaka kuona mabadiliko na ushirikiswaji wa vijana katika maendeleo ya jamii amesema 'kuna haja kubwa ya vijana sasa kushiriki moja kwa moja katika mabadiliko kwa kugombea nafasi mbali mbali za uongozi katika jamii"

LUKOSI alianza siasa rasmi katika Chama Cha mapinduzi mwaka 2012 na kwa bahati akapata nafasi ya kuchaguliwa kuwa mjumbe wa kamati ya serikali ya mtaa mwaka 2014 na sasa ameona ni muda sahii kwakwe kuwania kiti cha udiwani wa kata ya msasani.



Kuhusu kinachoendelea ndani ya chama chake na muelekeo wake katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu LUKOSI anasema kinachoendelea sasa katika Chama chake ni matokeo ya viongozi wajuu kutofata misingi iliyo wekwa na Baba wa taifa katika katika Chama na uongozi.

LUKOSI anatarajia kuchukua fomu ya kugombea kiti cha udiwani Alhamisi ya tarehe 16 july, siku ambayo itakuwa mwanzo wa kutengeneza mazingira mazuri kwa yeye kushinda kabla ya kura za maoni ndani ya chama ambayo yatatoa mwakilishi mmoja kutoka Chama Chake kugombea udiwani wa kata hiyo.


Anatoa wito kwa vijana kushiriki katika vuguvugu la mabadiliko katika jamii kwa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za kiuongozi katika jamii  aki nukuu maneno ya kiongozi wa kwanza wa Ghana Kwame Nkurumah 'Opportunity and responsibility are the only ways of realizing individual and collective potential" kuwa kuna fursa nyingi ambazo vijana tunaweza kuzitumia ili kusababisha maendeleo katika jamii zetu.







 


No comments:

Post a Comment