Imeandikwa na Jay4.
Wahenga
walisema,” kwenye wengi pana mengi”. Ndio hali nimekutana nayo katika
wanafunzi wengi wa Chuo cha Tumaini Dar es Salaam. Katika uwingi wao nikakutana
na kijana shupavu, mcheshi kwa kila
mmoja, aliebarikiwa fikra za mabadiliko kuhusiana na Chuo cha Tumaini Dar es
Salaam. Alijibu maswali matano kiufasaha nilipomuuliza katika mahojiano.
1. Unaitwa
nani?
Kwa majina nafahamika kama JACKSON SIMON SHEKIGENDA, nipo mwaka wa
pili kitivo cha Rasilimali watu (HUMAN
RESOURCE MANAGEMENT). Napatikana katika mitandao ya kijamii kama FACEBOOK
kama SHEKI_JR na INSTAGRAM
kama SHECK DIASPORA.
2. Ni
kitu gani umekiona muhimu katika vyuo vikuu vingine na ungependa kiwe miongoni mwa
huduma katika Chuo cha Tumaini?
Akiwa katika maandalizi ya mitihani ya mwisho.( Picha na Jay4) |
Kwa kutumia mfano wa Chuo kikuu cha
Dar es Salaam, kuna mambo mawili muhimu, la kwanza ni uwepo wa semina ambazo
hufanyika baada ya muda wa masomo darasani, zinaruhusu wanafunzi kuuliza
maswali na kueleza kiasi gani waeelewa. La pili ni kutokuwepo kwa hosteli,
wanafunzi tunapata tabu kwenda kupanga vyumba kwa bei ya juu tofauti na Chuo
kikuu cha Dar es Salaam ambao wana hosteli nzuri na zilizo ndani ya Chuo,
ningependa sana na hapa zijengwe hata kama si mimi niwe mtumiaji bali hata kwa
vizazi vinavyokuja katika Chuo hiki kizuri.
3. Kulalamikiwa
kwa sekta ya burudani Chuoni, unaishauri kipi serikali ya wanafunzi
(TUSODARCO)?
Kwanza tumekosa ushirikiano na vyuo
vingine ambavyo huwa na utaratibu wa kuungana na kuandaa burudani itakayotuleta
pamoja, kwahiyo uongozi lazima uweke ushirikiano na vyuo amabavyo vinaleta wanafunzi
pamoja katika burudani. Pia, wanafunzi tumetofautiana katika hulka ya kupenda
huduma tofauti katika burudani, kwa mfano mimi ni mpenzi wa muziki ningeshauri
kila baada ya mitihani watuwekee burudani ya muziki ‘kujipoza’ na mitihani.
4. Katika
huduma nyingi zinazotolewa na Chuo Cha Tumaini, Je huduma gani umeifurahia sana?
Nisiwe mnafiki, uongo dhambi.
Huduma ipo kubwa na sijui kama sehemu nyingine ipo, ni jinsi walimu
wanavyotujali katika ufundishaji wanakuwa kama marafiki, wanatupa taarifa na
uzoefu kadri ya uwezo wao ili kutufanya
kuwa wanafunzi bora zaidi. Ukaribu huu unanifanya nijisikie amani zaidi katika
masomo yangu.
5. Mwalimu
gani katika kozi yako unamuelewa sana?
Walimu wote nawaelewa ila zaidi
namuelewa Dr. Ngirwa, kwakuwa ni zaidi ya mwalimu namchukulia kama babu yangu. Vilevile nje ya darasa pia, hata uwe na tatizo
unaweza kumfata na akakupa ushauri mzuri sana. Kiukweli nampenda sana.
Umetishaa sana bruda.
ReplyDeletesafi sana..interview iko vzr sn
ReplyDeleteAsante wakubwaaa
ReplyDelete