Pages

Friday, October 30, 2015

MONK AMPA KIBARUA GOMIS HUKU WAWILI ARSENAL KUIKOSA SWANSEA

Bafetimbi Gomis (left) with Micah Richards

Baada ya kucheza michezo sita bila ya kufunga goli, kocha wa Swansea Garry Monk amegoma kumlaumu mshambuliaji wake ila amempa kazi ya kufunga katika mechi ijayo watakapowakaribisha Arsenal.
Gomis alianza ligi kuu kwa mbwembwe baada ya kufunga katika mechi zote nne aza awali na Monk anamlinda Gomis kwa kusema presha iko kwa kila mtu sio wafungaji pekee.
Bafetimbi Gomis
"Jumamosi sio tu kushinda bali kufanya vizuri katika sekta zote za timu yetu, cha muhimu zaidi ni kupata ushindi na yeyote atakaefunga ni jambo la msingi".

Mechi ya mwisho Swansea ilicheza dhidi ya ASton Villa na mwishoni kulishuhudiwa vitendo vya uvunjifu wa maadili katika vyumba vya kubadilishian nguo jambo lililoilazimu FA kuchunguza lakini hakuna adhabu yeyote iliyotolewa kwa mlinzi Micah Richards aliyevutana na Federico Fernandez wa Swansea. Wakati huo huo winga wa Swansea Wayne Routledge amerejeav rasmi mazoezini baada ya kuwa nje kwa muda kufuatia majeraha.
Theo Walcott
Kwa upande mwingine, Arsenal itasafiri hadi Wales bila ya wachezaji wake wawili wa muhimu kufuatia majeraha waliyoyapata katika mechi za katikati ya wiki za Kombe la Ligi.
Kocha Arsene Wenger alisema kuwa Theo Walcot na Alex Oxlade Chamberlaine watakosa mechi tatu za Arsenal na mbili za Uingereza kufuatia majeraha waliyopata katika kipigo cha 3-0 kutoka klabu ya daraja la kwanza ya Shelfied Wednesday.
Chamberlain aliumia misuli baada ya kucheza kwa dakika tano tu na Walcott kuingia kama mbadala wake kabla ya yeye pia kutolewa nje kwa majeraha ya kifundo cha mguu.

  



No comments:

Post a Comment