Pages

Thursday, October 29, 2015

LUKE SHAW AANZA MAZOEZI MEPESI CARRINGTON

                                                         Shaw steps up Manchester United comeback

Mchezaji wa Manchester United Luke Shaw ameendelea vizuri na safari yake ya kurudi uwanjani baada ya kuanza mazoezi mepesi katika kiwanja cha mzoezi chatimu hiyo cha Carrington.
Shaw aliumia katika mechi ya Ubingwa Ulaya baaada ya kuchezewa rafu mbaya na beki wa PSV, Hector jambo lililopelekea kuvunjika mara mbili kwa mfupa wa mguu wake.
Manchester United ina vifaa maalumu vinavyosaidia kupona haraka ambavyo ilivianzisha miaka miwili iliyopita kwa ajili ya kuwatibu wachezaji wake wanaopata majeraha ya muda mrefu. Vifaa hivyo ni kama swimming pool kubwa ya maji ya moto ambayo mchezaji hukaa ndani kwa muda ili kusaidia uponyaji wa majeraha yake na Shaw ameshaenda Carrington zaidi ya mara tatu sasa kwa wiki iliyopita.
Vifaa hivyo vina camera ambazo zinaweza kuona maendeleo ya jeraha la beki huyo wa kushoto alisajiliwa kama kinda ghali zaidi duniani akitokea Southampton misimu miwili liyopita.
.

No comments:

Post a Comment