Pages

Monday, October 12, 2015

JICHO LA WIKI; MAJERUHI WAONGEZEKA TIMU ZA TAIFA

Wikiendi hii kumekua na mechi mbalimbali za kufuzu michuano mikubwa ya mabara huku wachezaji muhimu wakipata majeraha ambayo yatawaweka nje kwa muda mrefu.
TIM KRUL NJE MSIMU MZIMA
Mlinda mlango wa klabu ya Newcastle na timu ya taifa ya Uholanzi Tim Krul amepata majeraha ya goti na imethibitishwa atakua nje ya uwanja kwa muda wote uliobakia wa msimu.
Kupitia ukurasa wake wa Tweeter, Krul alisema "Ninasikitikakusema kwamba majibu ya scan yameonyesha wasiwasi wangu mkubwa, naanza safari ya kurudi uwanjani sasa hivi kuelekea kupona".
Kipa huyo alipata majeraha hayo kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kazakhstan jumamosi iliyopita.
Akiwa na klabu ya Newcastle Krul amecheza michezo yote nane huku timu yake ikiwa mkiani mwa ligi ya Uingereza bila ya ushindi wowote.
GOTZE NJE WIKI 10-12
Mchezaji wa Germany na Bayern Munich Mario Gotze naye atakua nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa kuanzia wiki 10 hadi 12 kufuatia majeraha ya aliyopata wakati nchi yake ikiambulia kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Ireland katika mechi ya kufuzu michuano ya Ulaya 2016 itakayofanyika nchiuni Ufaransa mwakani June.
Mario Gotze
Kiungo huyo mwenye miaka 23 atakosa mechi kadhaa muhimu ikiwamo zote mbili za Champions League dhidi ya Arsenal, huku akiikosa pia Ujerumani itakapovaana na Georgie huku ikihitaji pointi moja tu kufuzu michuano hiyo. 
Gotze amefunga magoli manne hadi sasa akiwa Bayern na majeraha hayo yatamlazimisha kukosa nusu ya kwanza ya msimu wa Bundesliga.
KARIM BENZEMA, na wengineo.
Mshambuliaji wa Real Madrid Mfaransa Karim Benzema alifunga mabao mawili kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Armenia lakini furaha yake iliingia doa baada ya kutolewa nje kwa machela kufuatia majeraha ya misuli yaliyomkumba.
Alvaro Morata wa Juventus alitolewa nje kwa machela wakati nchi yake Spain ikivaana na Luxembourg baada ya kuangukiwa na mchezaji wa timu pinzani jambo lililozua mashaka kuwa atakua amevunjika mguu lakini majibu yaliyotolewa baada ya vipimo yalikanusha kuvunjika kwa mguu.
David Silva alitoneshwa majeraha yake ya enka kwenye ushindi wa 4-0 dhidi ya Luxembourg jambo litakalomuweka nje tena kwa muda huku akikosa mechi muhimu dhidi ya mashetani wekundu wikienmdi ijayo pale Old Trafford.
Sergio Aguero wa Argentina alitolewa nje kwa machela katika mechi ambayo timu yake ililala kwa mabao 2-0 dhidi ya Ecuador na atakua nje kwa wiki nne huku akiongeza msiba kwa Manchester City ambayo tayari itamkosa kiungo wake mahiri David Silva alieumia katika mechi za kimataifa.
Branislav Ivanovic wa Serbia ameendelea kuandamwa na zimwi baya baada ya kuanza msimu wa Ligi Kuu England vibaya na zimwi limeendelea kumtesa hadi timu ya taifa baada ya kutolewa nje kwa majeraha ya misuli.
Aleksandaer Kolarov wa Serbia na Manchester City alitolewa nje kwa majeraha ya misuli kwenye kipigo cha 1-0 kutoka Portugal kabla ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu alipojaribu kujitetea kwa waamuzi akitokea benchi alikolazwa baada ya kuumia.

No comments:

Post a Comment