Pages

Wednesday, October 14, 2015

VAN PERSIE AIUA UHOLANZI, YASHINDWA KUFUZU EURO 2016

Netherlands     

Uholanzi ilihitaji ushindi huku ikiomba Uturuki ifungwe na Iceland ili wapate nafasi ya kucheza mechi ya mtoano kwa ajili ya kufuzu michuano ya Euro 2016 itakayofanyika nchini Ufaransa lakini makosa ya Van Persie yaliigharimu timu hiyo kupoteza mechi katika ardhi yao hivyo kuua kabisa matumaini ya kufuzu michuano hiyo.
Van Persie alijifunga dakika ya 66 na kufanya timu yake kuwa nyuma kwa mabao 3-0 licha ya Jamhuri ya Czech kuwa na wachezaji 10 uwanjani kufuatia kadi nyekundu ya Mark Suchy.
Dutch supporters after their team's defeat in Amsterdam
Mashabiki wa Uholanzi wakitoka uwanjani kwa majonzi baada ya timu yao kushindwa kufuzu
Klaas-Jan Huntelaar na Van Persie walifufufa matumaini kwa kufung magoli mawili baada ya magoli ya uongozi kutoka kwa Pavel Kaderabek na Josef Sural lakini badala yake ni Uturuki ndio walishinda nafasi ya tatu baada ya kuifunga Icveland bao 1-0.
Wesley Sneijder
Kwa hali hiyo Uturuki wanafuzu moja kwa moja kwenda France kama timu ya juu zaidi ya nafasi ya tatu katika mechi zote tisa za kufuzu.
Matokeo mengine yalikua kama ifuatavyo;
 EUROPEAN CHAMPIONSHIP QUALIFYING
MON 12 OCT 2015 - EUROPEAN CHAMPIONSHIP QUALIFYING


No comments:

Post a Comment