Costa alifungiwa mechi 3 na FA baada ya kuanzisha ugomvi katika ushindi dhidi ya Arsenal alipogombana na Gabriel kabla ya Mbrazil mwenzake kutolewa nje kwa kadi nyekundu huku Costa akiachwa salama uwanjani kuendelea na mechi. Baadae kamati ya nidhamu ya FA ilikaa kikao na kumpunguzia adhabu Gabriel huku Costa akibeba adhabu ya kukaa nje mechi 3 jambo lililomgarimu Costa kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Spain wiki hii.
Chelsea itaivaa Southampton huku ikiwa kwenye hali mbaya baada ya kucheza mechi 11 kwa msimu huu na kupata clean sheet 2 tu huku wakiwa nafasi ya 15 baada ya mechi 7 wakiwa na pointi 8.
Radamel Falcao na Remmy wataanza katika mechi ya leo kuziba pemgo la Costa ambae ama,alizia adhabu yake kwa mechi ya leo.
Diego Costa akizuiwa na Ivanovic (kushoto) na Fabregas baada ya kuzuka tafrani kati yake na Fernandinho wa City (hayupo pichani) |
Mchezaji mpya wa Southampton Jordy Classie amerudi rasmi mazoezini baada ya kuwa nje kwa majeraha ya goti na anaweza kuanza mechi ya leo mchana.
Ryan Bertrand anatarajiwa kuanza dhidi ya timu yake ya zamani baada ya kucheza dakika zote 90 wikiend iliyopita baada ya kuumia goti msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment