Sunday, September 13, 2015
MESSI AIZAMISHA ATLETICO MADRID
Fernando Torres aliipatia timu yake ya utotoni goli la ufunguzi mapema baada ya kipindi cha pili kuanza lakini furaha yake ilidumu kwa dakika 5 tu kabla ya mshambuliaji wa Kibrazil Neymar kusawazisha kwa free kick.
Barcelona ,bayo haikuanza na m,shambuliaji wao Messi ilitawala sehemu kubwa ya mchezo huo lakini haikufanikiwa kupata bao katika kipindi cha kwanza.
Messi aliibuka mshindi kwa mara nyingine baada ya kufunga goli la ushindi dakika ya 77 na kuhakikishia ushindi wa 100% kwa mabingwa hao wa Katalunya.
Mar ya mwwisho kwa Messi kukaa benchi ilikua Januari mwaka huu dhidi ya Real Sociedad iliyo chini ya David Moyes, Barcelona iliishia kupoteza mchezo huo na kukazuka taarifa kuwa Messi hakua na maelkewano mazuri na kocha wake Luis Enrique jambo liliweka hatma ya kocha huyo katika wasiwasi.
Sasa Barcelona wameshinda mechi zote tatu kwa tofauti ya goli moja wakifanya hivyo kwa 1-0 pale Athletic Bilbao, 1-0 kwa Malaga na sasa 2-1 kwa Atletico.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment