Jinsi alivyoupokea mpira kutoka upande wa kushot na kusogea nao katika lango la Liver[pool kabla ya kumpiga chenga ya nje ndani beki nguli Skrtel kabla ya kuachia shuti lililopita pembeni ya kipa Mignolet na kuingia wavuni, inaonyesha dhahiri kuwa mvuto wa kwanza siku zote hudumu katika kumbukumbu za watu hasa mashabiki wa United.
Anthony Martial ameanza ligi kuu ya Uingereza kwa staili ya aina yake baada ya kufunga goli dhidi ya mahasimu wakubwa wa United, Liverpool.
Magoli ya awali kutoka kwa Daley Blind na penalti ya Ander Herrera yaliwapa Man United matumaini ya mechi hii lakini goli la tikitaka la Christian Benteke liliwapa wageni nguvu na kuonyesha uhai wa kutawala mechi kwa sehemu kubwa. Baad ya dakika 1 na ssekunde 56 tu. Anthony Martial alifunga goli la tatu akimaanisha hesabu za mechi hiyo muhimu zimefungwa.
Moja ya vichwa vya habari vya gazeti la Ulaya vikikandia hela iliyotumika kumnunua Martial. |
Goli la Martial limezaa matumaini kwa washabiki wa United juu ya mchezaji wao huyo mpya ambae amepewa jukumu la kucheza kama mshambuliaji kufuatia kuondoka kwa Mdachi Robin van Persie aliekimbiulia Fehnebarce ya Uturuki.
No comments:
Post a Comment