Manchester United inasafiri hadi nchini Uholanzi itakapomenyana na mabingwa wa nchi hiyo PSV. Hii inamrudisha mchezaji wao mpya, Memphis Depay katika klabu yake ya zamani iliomtengenezea njia kufikia alipo sasa. United itaenda Uholanzi bila ya mshambuliaji wao muhimu na kiongozi, Wayne Rooney aliyepata majeraha baada ya mechi za kimataifa akiwa na England.
Rooney hakuchezeshwa katika ushindi wa 3-1 dhidi ya mahasimu Liverpool na Van Gaal alisema hatma yake itaamuliwa baada ya mechi hiyo lakini ameamua kutomuweka hatarini ka kumchezesha dhidi ya PSV.
Andreas Perreira na James Wilson wamejumuishwa katika kikosi cha United kwa ajili ya mechi hiyo.
Sergio Aguero ataikosa mechi ya kwanza ya UEFA wakati Man City ikiikaribisha Juventus baada ya kuumia goti katika mechi iliyopita ya Ligi Kuu ya Uingereza alipoumizwa na Scott Dann wakati wakicheza dhidi ya Crystal palace.
Raheem Starling ameponamajeraha yake na atakuwepo kwa ajili ya mechi hiyo.
Aguero aliuumia goti mwezi Desemba mwaka jana jambo lililomuweka nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mzima.
Mpaka sasa Aguero amecheza mechi tano tu akifunga goli moja la ufunguzi dhidi ya Chelsea hapo 16 August.
No comments:
Post a Comment