Paul Pogba wa Juventus akiwania mpira na beki wa Lazio kwenye fainali ya SuperCoppa Italiana jioni hii mjini Shanghai, China. |
Juventus wameendeleza makali yao pale walipoachia msimu uliopita baada ya kuwafunga Lazio katika mcezo wa SuperCoppa Italiana uliofanyika nchini mjini Shanghai nchini China.
Wachezaji wapya Mario Mandzukic aliesajiliwa kutokea Atletico Madrid aliipa Juventus bao la kuongoza dakika ya 69 kabla ya mchezaji mpya mwingine Paulo Dyabala kuongeza la pili dakika nne tu baadae.
Juventus waliwakosa wachezaji wao muhimu kama Carlos Tevez, Arturo Vidal na Andrea Pirlo walioondoka Turin pamoja na majeruhi yaliyowaweka nje wachezaji wao tegemeo kama beki Chielini, Alvaro Morata na Sami Khedira. Kukosekana kwa wote hawa kuliipa matumaini Lazio kama kigezo cha kushinda mechi lakini Juventus ilikua imara na kupata ushindi mzuri katika kipindi cha pili cha mchezo.
Juventus walinyakua ubingwa wa kwanza wa SuoerCoppa Italia mwaka 1994-95 wakati Lazio walikua katika kampeni ya kuongeza SuperCoppa kwa mara ya saba. Kwa mara ya nne mfululizo mechi ya ufunguzi wa Ligi ya Serie A inachezewa nchini China.
Ushindi huo ni ishara nzuri kwa maandalizi ya ligi kuu ya Italia itakayoanza hivi karibuni huku Juventus wakijipanga kutetea ubingwa wao wa Scudetto.
No comments:
Post a Comment