|
WAYNE ROONEY NA MEMPHIS DEPAY WA MANCHESTER UNITED WAKISHANGILIA GOLI WALILOPATA DHIDI YA TOTTENHAM KATIKA MECHI YA UFUNGUZI WA LIGI KUU YA ENGLAND. |
Louis van Gaal amepata ushindi katika mechi ya kwanza ya msimu wa 2015-16 baada ya kuifunga 1-0 Tottenham Hotspurs, shukrani kwa bao la kujifunga la Kyle Walker aliejifunga akijaribu kumzuia Wayne Rooney aliekua mbioni kufunga dakika ya 22.
Manchester United ambao waliwatambulisha wachezaji wao wapya waliosajiliwa kiangazi hiki kwa kuanza kwa Depay, Schneiderlin, Damian na kipa Sergio Romero wakati kiungo wa kijerumani Schweinsteiger akiingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Michael Carrick.
Manchester United walipata nafasi nyingi kupitia kwa Ashley Young lakini walishindwa kupata goli la ufunguzi. Kipa David de Gea na kipa Hugo Lloris wa Tottenham wote hawakujumuishwa kwenye FIRST 11 za timu zao kwa majeruhi huku van Gaal akisema De Gea hayupo katika hali nzuri kiakili kuhusiana na sakata lake la kutaka kuhamia klabu ya Real Madrid linaloendelea baina ya timu hizo.
|
Harry Kane wa Tottenham akimiliki mpira wakati Daley Blind akipiga hesabu za kumkaba. |
Kipa mpya wa United Sergio Romero hakupata wakati mgumu sana kipindi cha kwanza lakini hali haikua nzuri kipindi cha pili wakati mchezo ukielekea mwishoni baada ya kuoka michomo miwili ilioelekezwa langoni kwake iliotumwa na Mdenmark Christian Erikksen.
|
David de Gea akifuatilia mechi ya timu yake dhidi ya Tottenham |
No comments:
Post a Comment