Pages

Monday, June 22, 2015

KILA LA KHERI KUELEKEA UNIVERSITIES EXAM

'Ukinicheka shambani mie nitakucheka sokoni'' msemo huu unatimia pale ambao baadhi ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali wakitarajia kufanya mitihani ya kumaliza mwaka wa masomo,kwani kumekuwa na tabia ya baadhi ya wanafunzi kuendekeza kula bata na kwa upande mwingine kuwacheka wenzao wanaopoteza muda wao kusongoka,kwa kuwaita majina mbalimbali ikiwemo vijukuu vya babu vilivyotumwa na kijiji.


 Wakati ambapo wanafunzi wa chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam wakiwa katika maandalizi yao ya mwisho mwisho kuingia katika mtihani huo unaotorajiwa kuanza mnamo tarehe 6 ya mwezi wa 7 mwaka 2015.


Habari zilizofika mezani kwetu zinaeleza  kuwa kuna baadhi ya vyuo vilivyoanza tayari kufanya mitihani yao ikiwemo chuo kikuu cha mtakatifu Augustino Mwanza,pamoja na chuo kikuu cha Jordan kilichopo Morogoro ambao kwa pamoja walianza siku ya jumatatu iliyopita.


Kwa upande mwingine habari tulizozipata kutoka vyuo mbalimbali, vikiwemo chuo kikuu cha Dar es salaam(mlimani)  na kile cha ardhi wao wanatarijiwa kuanza kufanya mitihani yao kuanzia siku ya jumatatu tarehe 22 mwezi wa 6 mwaka 2015.


 MAINKAMPASI inapenda kuungana na wasomi wote wa vyuo vikuu Tanzania kuwatakia kila la kheri, ndugu zetu waliopo kwenye mandalizi na wale wanaotarijia kuanza mitihani yao kwa siku za usoni.







No comments:

Post a Comment