Pages

Monday, June 22, 2015

TFF YAMTIMUA KOCHA STARS


MARTIN NOOIJ AKISINDIKZWA CHINI YA ULINZI WA POLISI

 Kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania maarufu kwa Taifa star,Muholanzi MARTIN NOIJ amefutwa kandarasi yake ya kuendelea kuifundisha timu hiyo hapo jana baada ya kuambulia kipigo cha tano mfululizo katika michezo mbalimbali ya timu hiyo iliyokuwa ikishuka dimbani,chini ya kocha huyo.

  Maamuzi ya kumtimu kocha huyo yalifikiwa jana usiku visiwani zanzibar na kamati ya utendaji ya shirikisho la soka Tanzania(TFF) ,mara baada ya timu hiyo kudondokea pua dhidi ya Uganda the cranes ,kwa kupata kichapo cha magoli 3 kwa sifuri katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufudhu mashindano yanayohusisha wachezaji wa ndani (CHAN).

 NOIJ alitimuliwa kutokana na muendelezo wa kupoteza michezo mitatu ya Cosafa dhidi ya swaziland,madagasca,lesotho pamoja na mchezo wa kuwania kufudhu mashindano ya Afrika (AFCON) dhidi ya Misri.

 Mpaka hivi sasa taarifa za chini kutoka shirikisho hilo zinadai kuwa  makocha wazawa BONIFACE MKWASSA(master) pamoja na HEMED MORROCO ndio wanapewa nafasi kubwa ya kuifundisha timu hiyo.Iliyopoteza umaarufu wake tokea alipoondoka mbrazili MARCIO MAXIMO.

KIKOSI CHA TAIFA STARZ KILICHOKUWA CHINI YA KOCHA MARTIN NOIJ.

No comments:

Post a Comment