Tuesday, November 17, 2015
HISPANIA VS BELGIUM IMEAHIRISHWA KUTOKANA NA SUALA LA USALAMA
Mechi ya kirafiki kati ya Uhispania na Ubelgiji imesogezwa mbele kutokana na wasiwasi unaoxidi kutanda juu ya suala la usalama baada ya Shambulio la Paris ambalo lilitokea karibu na uwanja wa taifa wa Ufaransa.
Shambulio la Paris liliua mamia ya watu huku mlipuko wa bomu ukitokea karibu ya Uwanja wa Taifa wa Stade de France ambapo mechi baina ya wenyeji na Ujerumani ilikua ikiendelea.
Chama cha Soka cha Ubelgiji kimesema imechukua maamuzi ya kufuta mchezo huo ambao ulipangwa kufanyika kwenye uwanja wa King Baoudin katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Polisi walimtaja mmoja wa washutumiwa wa shambulio la Paris, Salah Abdeslam, 26, ambae ni mzaliwa wa Brussels kama ndiye mkuu wa tukio hilo hivyo jambno hilo linaweza kuhatarisha usalama wa wanasoka wote wa nchi hizo mbili pamoja na mashabiki.
Wakati huo huo Chama Cha Soka Cha Ufaransa kimeamua kuendelea na ratiba zake kama kawaida wakati huu ambapo timu yao ya Taifa ikiwa katika mechi za ki=rafiki kujiandaa na michuano ya Euro 2016 itakayofanyikia hapo hapo Ufaransa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment