Pages

Tuesday, November 17, 2015

EURO 2016 KUFANYIKIA UFARANSA LICHA YA SHAMBULIO LA PARIS

 Allianz Riviera stadium in Nice


Chama cha Soka barani Ulaya, UEFA kimethibitisha kuwa michuano ya Euro 2016 itaendelea kama ilivyopangwa awali licha ya shambulio la kigaidi la Paris ambalo lilioshuhudia Wafaransa 129 wakipoteza maisha yao.
 Katika taarifa waliyoitoa juzi jumatatu, UEFA wamesema kwa miaka mitatu wamekua wakishirikiana na mamlaka za usalama kuhakikisha hali inakua nzuri kipindi cha michuano hiyo.
Droo kwa ajili ya michuano hiyo zitapangwa mnamo December 12 jijini Paris huku wasimamizi wa michuano hiyo wakisema kusimamisha michuano hiyo itakua ni kucheza mchezo wa kigaidi.
Ufaransa itacheza na Uingereza Jumanne hii katika mechi ya kirafiki ambayo nahodha wao kipa Hugo Lloris amesema siyo mechi ya kawaida kufuatia kumbukumbu mbaya ya shambulio la Paris.


No comments:

Post a Comment