Pages

Tuesday, July 7, 2015

PROFILE YA RAISI MSTAAFU KAUME KAUME




Imeandaliwa na Jay4
Penye wakati, usipitishe nyakati’ ndio msemo wa busara niliokutana nao kwa kijana mchapakazi na mwenye kipaji cha kutumia akili katika Chuo Kikuu cha Tumaini Dar es Salaam. Ameitumikia serikali ya wanafunzi (TUSODARCO) kwa kipindi cha mwaka 2014-2015 akiwa na cheo cha Raisi. Kwa muda mchache wa mahojiano alikuwa na haya ya kunieleza katika maswali matano niliyomuuliza.
Raisi mstaafu Kaume katika kikako. Picha na Jay4
1.      Unaitwa nani?
Naitwa Mheshimiwa Kaume George Kaume. Nasoma kozi ya Rasilimali watu na Utawala wa Biashara (Bachelor of Human Resources management and Bussiness administration) mwaka wa tatu.
2.      Je katika kipindi cha uongozi wako ni changamoto gani kubwa mbili ulikutana nazo?
“Ok asante kwa swali zuri, kwanza kabisa ni mazingira kwa ajili ya kuendeshea miradi ya serikali ya wanafunzi. Mfano tulitaka fungua mradi wa Kibanda kwa ajili ya kuuza vitafunwa na vinywaji ila ilishindikana, tulitaka kuweka na steshenari itakayoweza kuwa na huduma ya intaneti ndani ila ilishindikana pia. Nakili kuwa tulishindwa kutokana na mazingira hayakuwa rafiki kuweza kufanikisha haya yote. Changamoto ya pili kubwa ilikuwa ni hali duni ya kifedha katika serikali ya wanafunzi wakati nimekabidhiwa ofisi. Nathibitisha wazi kuwa nilipokea ofisi ikiwa na kiasi cha pesa taslimu za Kitanzania laki nane , ni ngumu kuendesha serikali kubwa ya Chuo kwa kiasi hiki kidogo ila nimejitahidi sana mpaka kufikia kukabidhi ofisi kwa uongozi mpya wa Mheshimiwa Khalifa Said ikiwa na kiasi kikubwa cha pesa taslimu milioni 16”.  
3.      Unajivunia mafanikio gani katika uongozi wako?
“Mosi najivunia kufanya jambo ambalo hata uongozi wangu ulishangaaa, ni kuona mabadiliko makubwa mpaka kufikia hatua ya kukabidhi serikali ikiwa na kikasi kikubwa cha fedha. Najiona ni shujaa sana. Pili ni kusaidia wanafunzi wasiojiweza kwa matatizo mbalimbali kama vile ada na kuwachangia matibabu na pesa ya kujikimu kwa asilimia kubwa”.
4.      Ushauri kwa serikali iliyopo madarakani kwa sasa na zijazo pia?
“Nina mambo kadha wa kadha kuwashauri ila muhimu ni kama wahenga walivyosema ‘kumbukumbu ya mfa maji, hubaki vichwani mwa samaki’ nikimaanisha siku zote wasimame, ili kumbukumbu yao iandikwe kwenye vitabu lakini wakifeli kuongoza kumbukumbu yao haiwezi dumu kwa muda mrefu mbele ya masikio ya familia kubwa ya Chuo cha Tumaini. Pia watambue serikali ni watu na watu ndio serikali, viongozi ni wasimamizi wa serikali, ukisimama kwenye mstari hutashindwa kuona nywele za mtuwa mbele yako”. Mungu awasimamie kwa kila jambo jema walifanyalo kwa maendeleo ya Chuo”.

Raisi MStaafu Kaume George Kaume. Picha na Jay4

      5. Huu msemo wako wa ‘penye wakati, usipitishe nyakati’ una maana gani?
(kwa kicheko cha juu sana).. ” una maana kuwa kwa uongozi huu uliopo na mwana Tudarco yoyote utakapo ona huu ni wakati wa kufanya jambo Fulani kwa ajili ya maendeleo ya chuo basi wafanye hapo wasisubiri kesho”.

No comments:

Post a Comment