Pages

Tuesday, February 9, 2016

ZOUMA NJE MIEZI SITA

Kurt Zouma

Beki wa klabu ya Chelsea, Mfaransa Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa kufika miezi sita kufuatia jeraha la goti alilopata katika mechi ya weekend hii dhidi ya Manchester United.
Zouma aliumia goti lake wakati akigombea mpira na kiungo wa United Michael Carrick na madaktari wamethibitisha atalazimika kufanyiwa upasuaji.
Katika akaunti yake ya Twiter Zouma alithibitisha kuumia kwa goti lake na kwamba upasuaji utafanyika muda wowote hivi karibuni huku akiwashukuru watu wote ambao wamekua wakimtumia message za pole.
Kwa maana hiyo Mfaransa huyo atakosa michuano ya Ulaya ambayo itafanyikia nchini kwake hapo baadae June akiwa ameshacheza mechi mbili za timu ya Taifa toka aitwe kwa mara ya kwanza.
Wachezaji mbalimbali wameendelea kumtumia salamu za pole na kumtakia pone haraka huku wakiongozwa zaidi na wachezaji wa Ufaransa.
Kiungo wa United, Morgan Schneiderlin aliandika katika ukurasa wake wa Instagram "Pole sana kwa kuumia, natumaini utarudi tena ukiwa imara zaidi".
Zouma lijiunga na Chelsea akitokea klabu ya St Ettiene ya Ufaransa katika dirisha la mwaka 2014 na ametengeneza ukuta mzuri pamoja na mkongwe John Terry ambae amethibitisha kuiacha klabu hiyo baada ya msimu huu.

No comments:

Post a Comment