Pages

Saturday, July 18, 2015

HAKUNA MAREFU YASIYOKUWA NA NCHA



Kiongozi wa darasa TIzibzomo Bernard (kushoto) akiwa na baadhi ya wanafunzi wenzake

“Kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho”  hayo yalikuwa ni maneno ya wanafunzi  wa Chuo Kikuu cha Tumaini jijini Dar es Salaam kutoka katika kitivo  cha  sanaa na sayansi ya jamii (FACULTY OF ARTS AND SOCIAL SCIENCES )  Idara ya mawasiliano kwa umma (DEPARTMENT OF MASS COMMUNICATION), mara baada ya kumaliza mitihani yao  ya mwisho, na wakisubiri mahafali ya kuhitisha elimu yao ya shahada ya mawasiliano kwa umma ya miaka mitatu.

Kutokana na furaha yao kuwa pomoni, ikapelekea kushindwa kuelezea siri ya mafanikio yao.  Kwani kila mmoja amesema ni “Mwenyezi Mungu pekee ndiye aliyefanikisha safari yao”. Ni darasa pekee lenye historia kubwa sana kwani ndilo lilimtoa raisi wa kwanza wa chuo Mwanamke ambaye ni Beatrice Kasambula, kitu ambacho hakijawai kutokea miaka yote ya nyuma tangu kuanzishwa kwa chuo hicho. Miongoni mwa kauli mbiu zake ni kuwa “wanawake wanaweza bila ya kuwezeshwa” kauli mbiu hiyo ndiyo iliyomuwezesha kushinda nafasi ya makamu wa raisi pamoja na nafasi ya uraisi baadae.
 
 Beatrice Kasambula Raisi wa kwanza mwanamke  chuo kikuu Tumaini
Mheshimiwa aliongea mengi, akiwa kama raisi wa chuo alifanya mambo makubwa ikiwa ni pamoja na kuwakopesha na kuwalipia wanafunzi karo kupitia serikali ya wanafunzi kwa wale waliokuwa hawajiwezi, kuleta ushirikiano mzuri miongoni mwa wanafunzi na kuondoa tofauti zao za kitivo kimoja na kingine, na kuhakikisha katiba ya chuo cha Tumaini inakamilika na hatua iliyopo sasa ni kupigiwa kura ya maoni tu (referendum) ili iweze kutumika, chini ya uongozi wa waziri wake wa sheria Bwana Muga ambaye kwa sasa ni muhadhiri katika chuo kikuu cha Tumanini Dar es Salaam.

Hata hivyo kiongozi wa darasa ambaye ni shupavu na mwenye bidii bwana Tzibazomo Bernard, alisema “siri pekee ya mafanikio ni kuwa na bidii pamoja na nidhamu” pia aliongeza kuwa anajivunia chuo cha Tumaini kwani kinatoa shahada nzuri ambazo zinasoko, uwepo wa majengo mazuri yanayokidhi, pamoja na sehemu za kujadiliana (vimbweta) ambapo hapo awali khali ilikuwa tofauti. Kila mmoja kwa namna yake alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa  yote aliyomtendea.

No comments:

Post a Comment