Imeandaliwa na Jay4
Uchaguzi mkuu wa Raisi, wabunge na madiwani
unakaribia ikiwa imebakia miezi kadhaa kufikia 25 Oktoba 2015. Wengi wamekuwa
na maswali kichwani juu ya uandikishaji wa njia ya elektroniki (Biometric Voters Registration) kama
itaweza kuandikisha Watanzania wote kwa muda uliopangwa. Mwanafunzi mahiri wa
sheria anatoa majibu kuhusu mambo muhimu ya Uchaguzi mkuu na taaluma yake.
1.
Unaitwa nani?
Kwa
majina yangu ya cheti nafahamika kama EPHANIA PIUS TOWO, nasomea kitivo cha
Sheria mwaka wa pili. Natumia mitandao ya kijamii pia napatikana INSTAGRAM:
FANIATOWO pia na FACEBOOK: EPIPHANIA
TOWO.
2.
Uandikishwaji mpya wa elektroniki kwa wapiga kura (BVR) hususani kwa wanafunzi walioko Chuoni na muda
wa Uchaguzi wanakuwa likizo ni haki?
“Hapana
si HAKI, kwanza ni nafasi kubwa ya kunyimwa haki ya kuchagua na kuchaguliwa
kama Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyosema katika kifungu cha 21. Kwanza muda
wa Uchaguzi wanafunzi wengi wanakuwa wako likizo majumbani kwao na wengi
wanakuwa wametoka mikoa ya mbali tofauti na chuo wanaposomea. Muda ni mdogo kwa
uandikishaji na hata kipindi cha uandikishaji wanafunzi tunakuwa katika kipindi
cha masomo, serikali haileti usawa kwa kuwafikiria wanafunzi waliotoka ile
mikoa iliopitiwa mfano Njombe, Lindi na Mtwara”.
3.
Kwa taaluma yako ya sheria unaishauri
nini Kamati ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)?
“Ushauri
mkubwa ni kuwepo sheria yenye kutambua Kitambukisho maalumu ambacho mwanafunzi atakipata kwa muda awapo
chuoni na kumfanya apige kura mahala popote bila kuvunja sheria za upigaji kura
mfano, kupiga kura mara mbili. Hii itasaidia kuendana na muda na kuwapa haki
wanafunzi wa vyuo vikuu wote.”
4.
Kwanini kuna ufinyu wa namba ya wanafunzi wa kike katika “Law school”?
“Hilo
ni jambo kiukweli linaumiza, tunakuwa wengi sana katika ngazi ya shahada ila
inapofikia ‘Law school’ namba kubwa inakuwa ni wanaume. Wengi huwa ni woga
katika masomo ya ngazi hii kwa kupewa vitisho na waliotangulia katika ngazi
hiyo japo sina uhakika sana. Ushauri kwa wanawake wote ni kupambana na
kuhakikisha tunafika ‘Law school’ ili tuweke usawa katika jamii yetu hususani
mawakili na wanaharakati amabapo wanaume wametawala sana”.
5.
Unavutiwa na mwanamke gani maarufu hapa
Tanzania?
“Dr.
Asha-rose Migiro ni mwanamke natamani kuwa kama yeye au kuwa zaidi yake haswa
katika sifa zote aliyoipa Tanzania na kutochoka katika uwajibikaje wa kazi za
kila siku. Uhodari wake unanifanya kunivutia zaidi kufata nyayo zake”.
Tupo vizuri sana lets keep this spirit up and up people, hurray
ReplyDeleteAsante sana mkuu, tutafikia malengo 1 day
ReplyDelete