FIFA inachunguza uhamisho wa mchezaji Eliaqium Mangala alietokea FC Porto kwenda Manchester City katika dirisha la usajili la mwaka jana.
Mangala, 24 alijiunga na City kwa ada inayoeleweka ni pauni milioni 32 huku akisaini mkataba wa miaka mitano.
Uhamisho wa Mfaransa huyo unaonekana kuvunja sheria za umiliki wa tatu wa mchezaji. Report hiyo inaonyesha kuwa FC Porto iko katika hali ya wasiwasi kuhusiana na uhamisho huo zaidi kuliko Manchester City.
Wao Manchester City hawana taarifa kama kuna uchunguzi wowote unaoendelea kwa sababu sheria za ligi kuu ya Uingereza inazuia umiliki wa tatu wa mchezaji katika madirisha ya usajili.
Mangal alianza safari yake ya kisoka na Standard Liege mwaka 2008 huku akishinda taji la ligi kwenye msimu wake wa kwanza kabla ya kuhamia Porto mwaka 2011.
Akiwa na Porto, Mangala ameshinda mataji mawili ya Ligi ya Ureno na kuitwa kwenye kiikosi cha Ufaransa kilichopigwa 1-0 na Uruguay June 2013.
No comments:
Post a Comment