Pages

Saturday, October 24, 2015

MESSI NJE TOP 10 YA BIDHAA BORA ZA KIMICHEZO

 Messi drops out of Forbes top 10 most valuable athletes list


Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina na Barcelona, Leonel Messi ametupwa nje kwenye kumi bora ya bidhaa bora za kimichezo katika ripoti iliyotolewa hivi karibuni na jarida maarufu la Marekani la Forbes.
Mara ya mwisho Messi alikua nafasi ya 9 mwaka 2014 akiwa na utajiri unaokadiriwa kufikia thamani ya $12 million - akishuka kwa milioni moja tofauti na mwaka juzi, amekosekana kwenye kumi bora ya mwaka huu.
Mcheza gofu Rory McIlroy na mwanamasumbwi Floyd Mayweather Jr wameingia top 10 hiyo huku Mayweather akisaini mikataba kibao yenye fedha nyingi kabla ya pambano lake na Manny Pacquiao mwezi July.
Staa wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo, aliyekua nafasi ya 7 mwaka jana, pia ameshuka kwenye viwango hivyo akianguka nafasi ya nane licha ya kuzindua bidhaa zaken za nguo.
Mahasimu wa La Liga, Real Madrid na Barcelona walishika nafasi ya tatu na ya pili mwaka jana lakini mwaka huu mambo yamekua tofauti baada ya kuangukia nafasi ya 5 na 7 huku Manchester United na Bayern Munich pia wakikamilisha list hiyo ya kumi bora.

No comments:

Post a Comment