Baada ya kurekodi ushindi wa asilimia 100 katika michezo ya kufuzu Euro 2016, England itavaana na Uholanzi kwenye dimba la Wembley katika mechi ya kirafiki hapo March 29 mwakani kama sehemu ya maandalizi kuelekea michuano ya Ulaya.
Kikosi hicho cha Roy Hodgs kitawaalika vijana wa Danny Blind hapo 29 March katika mechi ya kwanza toka wakutane February 2012.
England watasafiri hadi kwa mabingwa wa Ulaya, Spain kabla ya kuwaalika Ufaransa mwezi ujao,kisha watasafiri kwenda kwa mabingwa wa dunia Germany, March 26.
England wamefuzu kwa ajili ya michuano ya Euro 2016 kwa asilimia 100 rekodi ya kushinda mechi 10 kwenye mechi 10 ingawa Uholanzi imeshindwa kufuzu michuano hiyo.
No comments:
Post a Comment