Pages

Friday, August 21, 2015

VAN PERSIE AGUSA MPIRA MARA MBILI TU, AFUNGA GOLI LA USHINDI



Robin van Persie aliifungia timu yake mpya bao lake la kwanza na la ushindi katika mechi ya kwanza ya kufuzu kombe la Europa dhidi ya Atromitos Athens ya nchini Ugiriki.
Van Persie alietokea Manchester United msimu huu, aliingia dakika ya 80 na mpira wake wa kwanza kugusa ulizaa goli muhimu mnamo dakika ya 89 katika mechi ya hatua za mtoano za Europa Cup.
Van Persie aligusa mpira mara mbili tu, wa kwanza ulikua goli alilofunga kwa kichwa.
Tangu amehamia Uturuki Van Persie amehaha kupata goli la kwanza baada ya kucheza kwa jumla ya daika 63 tu katika mechi tatu kufuatia maumivu ya ugoko.

No comments:

Post a Comment