Pages

Saturday, October 24, 2015

AGUERO, SILVA, NASRI, DELPH KUIKOSA UNITED KESHO

China president Xi Jingping (left) and Prime Minister David Cameron (right) with Sergio Aguero
Aguero akipiga selfie na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameroon na Rais wa China, Ji Xpin baada ya viongozi hao kutembelea kambi ya mazoezi ya timu hiyo.
Wakati timu zote mbili za mji wa Manchester zikijiandaa kwa ajili ya Derby ya 170, City itawakosa wachezaji wake muhimu ambao wako nje kuugulia majeraha waliyoyapata katika mechi za kimataifa wiki chache zilizopita.
Mshambuliaji wao wa kutumainiwa Aguero hatakuwepo uwanjani kwa muda wa wiki 4 huku kiungo wao mahiri Davd Silva nae akiuguza majeraha yake ya enka. City pia itaendelea kuwakosa wachezaji wake wengine ambao ni Fabian Delph, Gael Clichy na winga wa zamani wa Arsenal Samir Nasri.
Akizungumzia kitendo cha kuendelea kumuweka benchi njahidha wake, kocha Pellegrini alisema ana mahusiano mazuri na beki huyo na kuahidi kuwa ni vizuri akapata muda wa kutosha kujiandaa kabla hajarudi kikamilifu kwenye game.
Kompany aliingia kuchukua nafasi ya kiungo  Mbelgiji mwenzie De Bruyne kwenye mechi ya Ligi Mabingwa Ulaya jumatano hii katika dakika za majeruhi.


No comments:

Post a Comment