Hakika
kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho asilani,msemo huu umetimia siku ya jana baada ya wapenda
soka wote duniani wakishuhudia kufungwa kwa pazia la mashindano ya kopa Amerika yaliyokuwa
yakitimua vumbi huku nyasi za viwanja
mbalimbali nchini Chile zikipatakukiona cha mtema kuni.
Mashindano hayo yalinogeshwa
kwa ushiriki wa timu za Bolivia,Chile,Peru,Uruguay,Colombia,Paraguay,Brazili,Mexico,Jamaica
na Argentina na nyingne nyingi yaliyaanza kwa kupooza lakini kadri siku zilivyokuwa zinasonga
mbele ndivyo yalipopata kujizolea umaarufu kutokana na vituko kadha wa kadha sambamba
na ufundi wa hali ya juu ulikuwa
unaonyeshwa na vijana kutoka bara hilo linalopatikana kusini mwa Amerika.
Kubwa zaidi ni kumuhusu kiungo wa timu ya taifa ya Chile na
klabu ya Juventus ARTULO VIDAL kukamatwa kwa kusabisha
ajali kutokana na unywaji wa pombe kupindukia siku chache kabla ya michuano hiyo kuanza,licha ya gari lake
kuharibika vibaya lakini mwenyewe hakupatwa na majeraha yoyote.Tukio hili lilikuwa
ni kama ndimu kwenye mchuzi kwani kwa upande wa pili liliwavutia wadau wa
kandanda haswa wakitaka kufahamu wenyeji hao wengefanya yapi katika michuano hiyo.
Mshambuliaji wa timu ya Argentina Lionell Messi akishangalia bao. |
Utamu wa mchuzi huo ulisabisha macho ya wapenda soka kuelekezwa kwa nyota wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina si mwingine ni Yule mchezaji aliyezaliwa na kipaji kikubwa ch kusakata kabumbu LIONELL MESSI, licha ya kufikisha michezo 100 pamoja na kuchangia timu yake kuelekea fainali,Kwa upande mwingine alishindwa kuisadia Argentina kutwaa ubingwa huo waliounyakua kwa mara mwisho mnamo mwaka 1993.
Shombo liliingia katika mchuzi huo pale beki wa Chile na klabu ya mainz
04 GONZALO JARA kuwatibua wapenda soka kutoka na kitendo chake kisichokuwa cha
kiungwana,mara baada ya kumchoma kidole mshambulia hatari wa Uruguay na PSG ya
Ufaransa mkali EDINSON CAVANI.Kitendo hicho
kilimpelekea beki wa Atletico Madrid DIEGO GODIN kulitaka shirikisho la soka
barani humo kutoa adhabu kali kwa JARA, kama ilivyokuwa kwa LUIS SUAREZ pale
alivyomngata beki wa Italia GEORGIO CHELLIN.Khali ilikaa sawa baada ya beki huyo kufungiwa kushiriki
michezo iliyobakia ya timu yake.
Gonzalo Jara akionyesha utovu wa nidhamu kwa cavani. |
Upekee wa mchuzi huo uliwashangaza wapenda soka na kuwaacha vinywa wazi
pale waliposhuhudia Chile ikitwaaa kombe lake la kwanza katika historia ya soka
ikiwa na wachezaji wenye viwango vya kisasa kama ALEXIS SANCHEZ anayekipiga na
washika mitutu wa ARSENAL pamoja na kiungo mpambanaji ARTULO VIDAL ambaye
unaweza kumfananisha na yule mkali wa sinema za
kivita SILVESTER STALLON wengi wanamuita
RAMBO.
Chile walinyakua ndoo hiyo baada ya kuisukumiza nje ya
mashindano hayo Argentina kwa mikwaju ya penalti 4 kwa 1 baada ya dakika 120 za mchezo huo
kumalizika timu zote zikiwa suluhu ya kutokufungana.Argentina iliyokuwa chini ya kocha TATA MARTINO watajilaumu kwa kukosa
ubingwa huo licha ya kumiliki kikapu kilichokuwa
na nyota wasioweza kuhesabika wakiwemo ANGEL DI MARIA,GONZALO HIGUAN,HAVIER
PASTORE,LIONEL MESSI na SERGIO AGUERO.
Wachezaji wa timu ya Argentina wakijiaanda kupiga mikwaju ya penalti dhidi ya Chile. |
Penalti za mabingwa hao ziliwekwa kambani na
FERNANDEZ,VIDAL,SANCHEZ huku penalti ya kuondoa aibu kwa upande wa Argentina
ilisukumizwa kambani na MESSI
Mabingwa wa kopa Amerika 2015 Chile wakishereheka kombe lao. |
Mashindano hayo yalimaliza kwa Peru kuibuka kuwa timu yenye
nidhamu kwenye michuano hiyo huku EDUARDO VARGAS
tokea Chile na PAOLO GUERRERO kutoka Peru wakiondoka na kiatu cha
dhahabu baada ya kuibuka wafungaji bora kwa kuwa na jumla ya magoli manne(4)
kila mmoja.
Eduardo Vargas wa Chile akisherekea moja ya goli alilotupia. |
Hakika kwa wale mashabiki walevi wa mashindano haya tukutane
tena mwakani kule nchini marekani.Ila utakubaliana nami kuwa mashindano ya mwaka huu yalikuwa na utamu wa aina yake au sio???.TUKUTANE PALEE VIGOGONI KWA MASTORI MENGI MENGI.
Nembo itakayotumika katika mashindano hayo mwakani nchini Marekani. |
No comments:
Post a Comment