Bondia maarufu kutoka nchini Marekani ambaye anaeshikilia
rekodi ya kucheza michezo mingi ya masumbwi bila kudundwa brazameni na bishoo FLOYD MONEY MYWEATHER 38,amenyanganywa
ubingwa welterweight pamoja na kutokutambulika kama bingwa katika
shirikisho la ngumi duniani(WBO).
Myweather pichani akiwa na mataji yake matatu. |
Tukio hilo limetokana na MYWEATHER kuvunja
sheria zinazoungoza mchezo huo wa
masumbwi zilizomtaka,mosi kulipa ada ya ushiriki wa ubingwa huo kiasi cha $200,000 katika siku ya ijumaa
iliyopita kutokana pambano lake la mei 2
dhidi ya Mfilipino MANNY PACQUIAO .Pili kukiuka kanuni inayokataa bingwa wa
shiriksho hilo kupambana na kushikilia mikanda
ya uzani zaidi ya mmoja.
Myweather akimbonyeza mwenzie kizenji. |
Kabla ya kupokonywa ubingwa huo wa
(WBO) MYWEATHER alikuwa anashikilia mikanda ya uzani tofauti ikiwemo
welterweight kutoka WBC pamoja na ule wa
super welterweight kutoka shirikisho la WBA
Licha kupewa adhabu hiyo kamati ya shirikisho hilo imempatia kibali cha
siku 14 bondia huyo kukata rufaa kutokana
na maamuzi yaliyochukuliwa,kama kanuni ya za mchezo huo inavyoelekeza katika ibara
ya 34 ibara ndogo ya 3(e) ikiwa bondia
hajaridhishwa na maamuzi ya shirikisho hilo ataruhusiwa kukata rufaa kwa
kipindi kisichozidi siku 14 na kuiwasilisha kwa rais wa shirikisho hilo.
watoto wa mujini wanakwambia ni checheeeee.Myweather akikiona cha moto kutoka kwa Pacquiao. |
IKUMBUKWE ushindi wa mataji hayo matatu kwa bondia huyo
yalipatikana kimagumashi tarehe 2 ya mwezi mei dhidi ya PACQUIAO
ulikuwa ukilalamikiwa na wapenda masumbwi kote duniani ,Hivyo majanga hayo
yametafsiriwa kama ni matokeo ya laana kutoka kwa PAC
MAN.
IMELETWA KWENU:
KWA HISANI YA WATU KUTOKA KIBENCHI MAWAZO…011.
No comments:
Post a Comment