Wanafunzi wa chuo Kikuu Tumaini cha jijini Dar es salaam
wameulalamikia uongozi wa chuo hicho kutokana miundombinu mibovu ya vyoo chuoni
hapa hasa katika jengo jipya.
Wakiongea na mwandishi wa blogi hii,
mmoja wa wanafunzi Jumanne Muyonga anaesomea SHAHADA YA MAWASILIANO mwaka wa
pili amesema “nimepata shida sana kwani
kila ghorofa ninayoenda imefungwa na ilinibidi niende nje kwenye maliwato ya
zamani kupata huduma..
Kwa upande wa mratibu wa jengo hilo Bwana
Godfrey, amesema tatizo la kuziba kwa mabomba ya maji machafu ambayo lilitokana
na mifuko ya pombe maarufu kama viroba. na wametatua tatizo hilo na hakuna
shida tena wanafunzi wanaweza kuendelea kutumia kama kawaida.
Bwana Godfrey ametoa wito kwa wanafunzi na watumiaji wahuduma za maliwato kuwa
makini na kutunza miundombinu iliyopo kwani ikiharibika inatumika gharama kubwa
kuikarabati.
Mfano wa viroba vilivyo sababisha vyoo kuziba. |
Moja ya choo katika jengo jipya. |
No comments:
Post a Comment