Akiongea
na mwandishi wa Blogi hii, mmoja ya walinzi alisema “tumepewa majukumu mengi
sana ambapo ni pamoja na kuwakagua wanafunzi endapo wanavitambulisho halali vya
chuo au la, lengo ni kugundua yupi mwanafunzi na yupi si mwanafunzi. Lakini
baadhi ya wanafunzi wanakataa kukaguliwa na tukiwapeleka kwa Afisa Rasilimali
Watu Bw Mwita hawachukuliwi hatua yeyote”.
Kwa
upande wake afisa rasilimali watu Bw Mwita amesema walinzi hawawatendei haki
wanafunzi kwani kitendo cha kusahau kitambulisho ni kawaida kwa binadamu, hivyo
si utu kumzuia mwanafunzi kuingia ndani kwani wengine wanakua katika kipindi
cha mitihani.
Hata
hivyo wanafunzi nao wanawalaumu walinzi kwa kutokua makini na kazi yao. Wengine
wanasema wanafunzi hawafuati sheria za chuo na wanawatendea vibaya walinzi na
kuwadharau kutokana na kazi wanayofanya.
Mlinzi akiwa kazini
No comments:
Post a Comment