TUDARCO’S
Speakers bureau imepata viongozi wake
wapya ambao wamechaguliwa leo tarehe 19 mwezi wa sita 2015 majira ya saa 10:00
jioni katika chumba namba 801 ndani ya jingo
jipya la kisasa.
TUDARCO
SPEAKERS BUREAU, ni taasisi huru isiyofungamana na upande wowote wa kidini wala
wa kisiasa, malengo yake makuu ni kufanya midahalo pamoja na kuandaa mihadhara
mbalimbali ambayo itakua na manufaa kwa wanafunzi,na kuwajengea wanafunzi kujiamini na kuongea mawazo
yao mbele ya umati mkubwa wa watu ndani na nje ya chuo.
Viongozi
hao wapya ni pamoja na Meshack King’ani
ambae ni Mwenyekiti na makamu wake ni Mapinduzi
Kiongore. Pia kuna nafasi ya katibu ambayo imechukuliwa na Mahenge Majige na makamu wake ni Itanisa Asela na kuna nafasi ya muhasibu ambayo imecukuliwa
na Hajra Khatibu na msaidizi wake ni
Nasibu Mahinya.
Viongozi
hao wapya wameahidi kutekeleza maukumui
hayo waliyopewa kwa khali na mali ili kuhakikisha malengo tarajiwa yanafikiwa,
pia wakasema watajitahidi kuhakikisha idadi wa wanachama inaongezeka.
Kutoka kulia ni Majige Mahenge (katibu mkuu), Hajra )Khatibu (muhasibu), Meshaki King'ani (Mwenyekitim Mapinduzi Kiongore (Mwenyekiti Msaidizi na Nasibu Mahinya |
Congrats to all
ReplyDelete