Pages

Saturday, June 27, 2015

VIJANA WAASWA KUMTEGEMEA MUNGU

Vijana  wameaswa kumtegemea Mungu katika maisha yao ya kila siku, hayo yamesemwa na Mwinjilisti Enaesh Makanza alie mwakilisha Mchungaji wa Usharika wa Msasani katika Mahafali ya Umoja  wa wananafunzi wakristu vyuo vikuu USCF Tawi la Chuo kikuu cha Tumaini Dar es salaam.


Akinukuu kutoka Biblia tatatifu kitabu cha Mithali 4:13 ambapo Neno hilo  linahimiza kumshika sana Elimu na wasimwache aendezake lakini Makanza alisema bila ya kumshika Yesu na kumtegemea Mungu maisha na Elimu vitakuwa havina faida yeyote katika maisha.

Pia Makanza aliwaasa viongozi wapya ambao pia waliwekwa wakfu katika mahafali hayo kumtegemea Mungu na kuwakumbusha kuwa Mungu wetu ni Mungu wa utaratibu na hivyo ni vyema kufanya kazi katika ushirika na makubaliano ambapo katika umoja ndipo Mungu anatenda kazi.

Mwinjilisti Enash Makanza akiongea na viongozi wapya (hawapo pichani)
Nae mlezi wa USCF tawi la Chuo Kikuu Cha Tumaini Dar es salaam Mchungaji Lukonge amesisitiza vijana kusikiliza sauti ya Mungu na kuachana na sauti za kidunia ambazo kwa sasa zimekuwa nyingi kupitia mitandao ya kijamii kama whatsapp, twitter na Facebook ambazo kama zitasikiwa vibaya zitasababisha uharibifu mkubwa kwa kijana.


Akinukuu kutoka katika Kitabu cha Mathayo 7:24-27 ambapo Biblia takatifu inasema yule asikiaye na kutenda maneno ya Mungu anafananishwa na mtu aliejenga Nyumba yake juu ya mwamba kupitia maneno ya mstari huu Mchungaji Lukonge alitilia mkazo zaidi juu ya kusikia na kutenda maneno ya Mungu maana kumtumikia Mungu kuna faida zaidi kama kujenga Nyumba yake juu ya Mwamba kama ata yasikia na kuyatenda yalio ya Mungu.

Mchungaji Lukonge akiwashika viongi wastaafu ishara ya kuwaaga

Akitoa nasaha za mwisho Mch Lukonge aliwasisitiza waagwa kuwekeza katika masoko ya mitaji na Ardhi ambazo ni Amana ya kudumu.

No comments:

Post a Comment