Pages

Sunday, June 28, 2015

KATI YA WEMA NA DIAMOND NANI MTANI JEMBE?.



Ukiwa ni mpenzi wa muziki wa bongo fleva utaukumbuka mstari wa wimbo huu ulioimbwa na JOSEPH HAULE a.k.a profesa  jay ‘Upinzani wa jadi bongo haupo kati ya Simba na Yanga kuna Denti na konda, mgambo na machinga”,Lakini hivi karibuni kumeibuka mpambano mwingine wa nani  mtani jembe kwenye tasnia ya burudani  katika mitando ya kijamii kati ya mashabiki wanaopenda kumfuatilia nyota wa filamu WEMA SEPETU(Team Wema) pamoja na wale wanaovutika kwa nyota wa muziki wa Bongo fleva Naseeb Abdul maarufu kama DIAMOND PLATNUMZ(Team Diamond).


Wema na Diamond kipindi wakiwa wapenzi.
Katika tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music  Award msimu wa  mwaka 2014,wakati nyota hao wakiwa katika mahusiano ya kimapezni,mchango na nguvu ya timu zao ulionekana bayana haswa pale DIAMOND alipowaacha midomo wazi waandaji wa Tuzo hizo baada ya kukomba tuzo sita katika vipengele vyote alivyokuwa amepangikiwa kuviwania.

Muendelezo wa  stori hii ulizidi kunoga baada ya kuripotiwa nyota hao kupigana chini na kila mmoja wao kuifuata njia yake huku DIAMOND akingia kwenye uhusiano na ZARRI  THE BOSS LADY kutoka nchini Uganda. Hali iliyopeleka nyota huyo kuchochea vita vikali vya maneno dhidi ya mashabiki wao.

Diamond akiwa na Zarri katika pozi.
Tuzo za KTMA  zilizofanyika mwaka 2015 mashabiki wa WEMA walionyesha kumpigia promo msanii ALI KIBA ambae ndiye aliyekuwa anaonekana mpinzani mkubwa wa DIAMOND.Mwisho wa mpambano huo KIBA kwa ushirikiano wa mashabiki wa Wema alifanikiwa kuchukua tuzo 6 huku diamond akiambulia mblili

Utafiti uliofanywa na Bongo 5  umetoka na orodha ya wasanii pamoja na watangazaji  3  bora wenye ushawishi mkubwa katika jamii  ambapo kauli zao sambamba na ushauri wanaoutoa kupokelewa na idadi kubwa ya mashabiki katika mitandao hiyo ya kijamii.


Nafasi ya tatu ilikamatwa na mtangazaji maarufu kutoka redio ya watu Clouds fm na mkali wa kipindi cha AMPLIFYA mtu wako wa nguvu MILLARD AYO.takwimu zinaonyesha mtangazaji aliwa na zaidi ya watu 40,000 wanaomfuta katika mitandao ya kijamii.Hivyo kuibuka kuwa mtangazaji anaependwa zaidi nchini kwa hivi sasa.Kutokana na kuwa mchapakazi,mcheshi na mtu anayependa kujituma.

Pichani Millard Ayo
Nafasi ya pili imekamtwa na DIAMOND PLATNUMZ ambaye nyimbo zake zimeelezewa kuwagusa watu wenye matabaka mbalimbali katika jamii ikiwemo maskini kitu kilichosababisha nyimbo zake kuvuja na kupigwa sana mtaani zikiwa bado hazijafika kwenye vyombo vya habari nyimbo kama Mbagala,ukimwona nataka kulewa na nitampata wapi.Takwimu zinaonyesha platnumz ndiye msanii pekee anayeongoza kwa kupiga shoo nyingi na kulipwa zaidi,habari zandani kutoka kampuni ya push mobile zinadai kuwa Diamond ndie msanii anayeongoza kwa nyimbo na kwa kulipwa fedha nyingi pamoja na kupendwa  kutokana nyimbo zake kufanya vizuri zaidi katika miito ya simu.


Diamond platnumz
Nafasi ya kwanza imekamatwa na WEMA SEPETU ambaye ashawahi kunyakuwa taji la miss Tanzania pamoja na kuwa mwigazaji wa daraja la juu Tanzania,hali inayopelekea vijana wengi kupenda kumfuatili kutokana na uzuri wake pamoja na kazi zake jambo lililomsaidia kuweza kuibuka kama msanii mwenye ushawishi mkubwa kwa sasa.

Wema Sepetu katika pozi

No comments:

Post a Comment