Pages

Friday, May 27, 2016

SEKUCo

Habari, Karibu katika Blog Mpya ya Habari na Burudani kwa wanachuo.

Wednesday, March 16, 2016

TANZIA

Serikali ya wanafunzi inasikitika kuwataarifu kifo cha mwanafunzi Eunice Mawala wa CERTIFICATE IN RECORD MANAGEMENT kilichotokea leo tarehe Machi 16,2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alikuwa anasumbuliwa na tatizo la moyo. Msiba upo Kimara Jijini Dar es Salaam.

Naomba tuungane na familia yake kwa kumwombea apumzike mahali pema peponi. Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe sasa na hata milele. Amina.

kwa taarifa zaidi tunaweza kuwasiliana kwa namba  0716 670298 na  0717 961245. kwa taarifa za mazishi tutajuzana pia.

Tuesday, February 9, 2016

ZOUMA NJE MIEZI SITA

Kurt Zouma

Beki wa klabu ya Chelsea, Mfaransa Kurt Zouma atakua nje ya uwanja kwa muda unaokadiriwa kufika miezi sita kufuatia jeraha la goti alilopata katika mechi ya weekend hii dhidi ya Manchester United.
Zouma aliumia goti lake wakati akigombea mpira na kiungo wa United Michael Carrick na madaktari wamethibitisha atalazimika kufanyiwa upasuaji.
Katika akaunti yake ya Twiter Zouma alithibitisha kuumia kwa goti lake na kwamba upasuaji utafanyika muda wowote hivi karibuni huku akiwashukuru watu wote ambao wamekua wakimtumia message za pole.
Kwa maana hiyo Mfaransa huyo atakosa michuano ya Ulaya ambayo itafanyikia nchini kwake hapo baadae June akiwa ameshacheza mechi mbili za timu ya Taifa toka aitwe kwa mara ya kwanza.
Wachezaji mbalimbali wameendelea kumtumia salamu za pole na kumtakia pone haraka huku wakiongozwa zaidi na wachezaji wa Ufaransa.
Kiungo wa United, Morgan Schneiderlin aliandika katika ukurasa wake wa Instagram "Pole sana kwa kuumia, natumaini utarudi tena ukiwa imara zaidi".
Zouma lijiunga na Chelsea akitokea klabu ya St Ettiene ya Ufaransa katika dirisha la mwaka 2014 na ametengeneza ukuta mzuri pamoja na mkongwe John Terry ambae amethibitisha kuiacha klabu hiyo baada ya msimu huu.

Saturday, February 6, 2016

VURUGU ZINGINE ZAIBUKA NCHINI SYRIA

 Syrian woman fleeing embattled city of Aleppo in Bab al-Salam, next to the city of Azaz. 5 Feb 2016


Mapambano makali yameibuka jirani na mji wa Allepo kaskazini mwa Syria wakati majeshi ya Serikali yakijaribu kuwazunguka waasi waliojificha katika mahandaki.
Kundi la Wachunguzi wa Haki za Binadamu la Syria limesema wanajeshi zaidi ya 120 kutoka katika pandezote mbili wameuawa kwenye mji wa Ratyan Ijumaa hii.
Zaidi ya wakimbizi 20, 000 walikimbia mapigano yanayoendelea wakijaribu kuvuka mpaka wa Syria kuelekea nchini Uturuki.
Uturuki imesema imejiandaa kuwasaidia wakimbizi ingawa mipaka imefungwa. Siku chache zilizopita majeshi ya Syria yalisaidiwa msaada wa silaha za anga na majeshi ya Urusi katika mji wa Allepo.
Ijumaa hii televisheni ya Taifa ya nchini Syria ilisema majeshi ya waasi yaliuteka mji wa Ratyan ulioko kaskazini kidogo mwa mji wa Allepo.

Friday, December 11, 2015

STUDENTS’ GOVERNMENT LEADERSHIP 2015/2016



  
TUSODARco president Rashid Khalifa


 The President of Tumaini University Dar es Salaam College, Rashid Khalifa  has amended his cabinet by reducing the number of Ministries and Ministers too.

The amendment was done on Thursday 9th December 2015 after seeing there was no need of having larger number of Ministries and Ministers because even few Ministers can work to the large extent.

“I need to work with few Ministers and their deputies, because I  believe the work done by few people is the best and I real believe on them  for your commitment of working with me” he insisted the President.

The new cabinet has, The General Secretary is Salama Mahmod, Rogers Somji  as a prime Minister,  the office of vice-president, finance and planning will be under The Vice President Steven Mjema as the supervisor and to  be run by Hebert Alli and Itanisa Asela as Minister and deputy Minister.

The ministry of Constitution and law will be under Fred Terasis as the Minister, also the Ministry of Good Governance and loan will be under Jumanne Paul and Kaijage Tabaro as Minister and deputy minister.

Also there is the Ministry of Education, Information and Communication will be under Mapunda Florid and Jane Yohane as the Minister and deputy Minister. And the last is the Ministry of Sports and entertainment and will be under Sakurani Baltazar.


                 STUDENTS’ GOVERNMENT LEADERSHIP  2015/2016

POSITION



NAME

TELEPHONE NUMBER

THE PRESIDENT


RASHID KHALIFA
0716 874 501
VICE PRESIDENT

STEVEN MJEMA
0655 553 388
THE PRIME MINISTER

SOMJI ROGERS
0719 059 950
THE GENERAL SECRETARY

SALAMA MAHMOD

0676 294 629
THE MINISTER OF LAW AND CONSTITUTION
FRED TARASIS
0759 701 064
THE MINISTER OF LOAN AND GOOD GOVERNANCE
JUMANNE PAUL
0719 072 050
THE DEPUTY MINISTER OF LOAN AND GOOD GOVERNANCE
KAIJAGE TABARO

0784 162 363
THE MINISTER OF EDUCATION, INFORMATION AND COMMUNICATION


MAPUNDA FLORID


0717 961 245
THE DEPUTY MINISTER OF EDUCATION, INFORMATION AND COMMUNICATION



JANE YOHANA


0656 119 363

THE MINISTER OF SPORTS AND ENTERTAINMENT

SAKURANI BALTAZAR

0653 077 840
THE MINISTER  OF FINANCE
ALI HEBERT
0658 012 305
THE DEPUTY MINISTER OF FINANCE

ITANISA ASELA

0719054 712

Sunday, December 6, 2015

PPF, TBL na NMB ZAKIMBIZA TUZO BORA ZA MAHESABU YA MWAKA.

Mwandishi wa Blog hii akiwa na Tuzo ya PPF ya Taasisi zilizowasilisha taarifa za mahesabu klwa mwaka 2014, kutoka bodi ya wahasibu na wakaguzi,NBAA.

Kampuni ya bia ya TBL ilichaguliwa mara ,mbili katika utoaji wa zawadi kwa taasisi zilizowasilisha taarifa za mahesabu kwa mwaka 2014 zilizotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) katika hoteli ya ACP Bunju jana usiku.
Kwenye upande wa Taasisi ya Uzalishaji TBL walishinda huku wakifuatiwa na Tanga Cement na Shirika la Sigara la TCC.
Wasindi wengine walikua ni kama ifuatavyo;
Kundi la Benki. mshindi NMB akifuatiwa na CRDB na DCB Commercial Bank.
Kundi la Biashara na Usambazaji; mshindi TTCL, akifuatiwa na CMC Motors na SwissPort Tanzania.
Kundi la Taasisi za Serikali zinazotumia mfumo wa IFRS; mshindi TRA, akifuatiwa na TBC na Bodi ta Pamba Tanzania.
Kundi la Taasisi za Udhibiti; mshindi ni Shirika la Anga (TCAA) akifuatiwa na SUMATRA na EWURA.
Kundi la Maji; Iringa Urban Water Supply mshindi akifuatiwa na Tanga Urban Water Supply.
Kundi la Serikali za mItaa; Hannag mshindi akifuatiwa na Ilala na Misenyi.
Kundi la Hifadhi za Jamii; PPF washindi wakifuatiwa na NSSF, LAPF.
Kundi la Universities; Chuo cha Sayansi ya Afya cha Roman Catholic cha CUHAS mshindi akifuatiwa na Ardhi.

Thursday, December 3, 2015

NEVILLE ATEULIWA KUIFUNDISHA VALENCIA

 


Beki wa zamani nguli wa klabu ya Manchester United, Garry Neville ameteuliwa kuiongoza timu ya Valencia inayoshiriki ligi kuu nchini Hispania, La Liga.
Maamuzi hayo yamekuja ghafla baada ya kocha aliekua akiifundisha timu hiyo Nuno Espirito Santo kuachia ngazi katikati ya msimu huku mechio ya kwanza ya Neville itakua dhidi ya Lyo, mechi ambayo lazima Valencia ishinde ili iweze kufuzu kwenda raundi ya mtoano ya Champions League.
Neville, 40 amemteua mdogo wake wa damu, Phil Neville kama kocha msaidizi baada ya Phili kujiunga na klabu hiyo katika benchi la ufundi mapema January mwaka huu.
Neville anakua mchezaji wa 29 kutoka katika utawala wa Ferguson kuwa kocha baada ya uteuzi huo. Sir Alex Ferguson alimpongeza Neville kwa uteuzi huo huku akimsifia kuwa ni kiongozi mzuri ndani na nje ya uwanja kwa hiyo itakua ni nafasi nzuri kwake kuonyesha ulimwengu wa soka kitu alichonacho kama kiongozi.
Naye Kocha wa timu ya Taifa ya England, Roy Hogson amempongeza Neville kwa hatua hiyo huku akisema kuwa nafasi ya Garyu katika timu ya taifa iko pale pale na haitaatiriwa na uteuzi huo. Garry amekua katika benchi8 la ufundi la England kwa muda sasa.
Wachezaji wengine waliofanikiwa kuwa wakufunzi kutoka katika kikosi cha Ferguson ni kama Viv Anderson, Michael Appleton, Henning Berg, Clayton Blackmore, Laurent Blanc, Steve Bruce, Chris Casper, Peter Davenport, Simon Davies, Darren Ferguson, Ryan Giggs, David Healy, Gabriel Heinze, Mark Hughes, Paul Ince, Andrei Kanchelskis, Roy Keane, Henrik Larsson, Gary Neville, Paul Parker, Mike Phelan, Bryan Robson, Mark Robins, Teddy Sheringham, Ole Gunnar Solskjaer, Frank Stapleton, Gordon Strachan, Chris Turner, Neil Webb.