Mwandishi wa Blog hii akiwa na Tuzo ya PPF ya Taasisi zilizowasilisha taarifa za mahesabu klwa mwaka 2014, kutoka bodi ya wahasibu na wakaguzi,NBAA. |
Kampuni ya bia ya TBL ilichaguliwa mara ,mbili katika utoaji wa zawadi kwa taasisi zilizowasilisha taarifa za mahesabu kwa mwaka 2014 zilizotolewa na bodi ya wahasibu na wakaguzi (NBAA) katika hoteli ya ACP Bunju jana usiku.
Kwenye upande wa Taasisi ya Uzalishaji TBL walishinda huku wakifuatiwa na Tanga Cement na Shirika la Sigara la TCC.
Wasindi wengine walikua ni kama ifuatavyo;
Kundi la Benki. mshindi NMB akifuatiwa na CRDB na DCB Commercial Bank.
Kundi la Biashara na Usambazaji; mshindi TTCL, akifuatiwa na CMC Motors na SwissPort Tanzania.
Kundi la Taasisi za Serikali zinazotumia mfumo wa IFRS; mshindi TRA, akifuatiwa na TBC na Bodi ta Pamba Tanzania.
Kundi la Taasisi za Udhibiti; mshindi ni Shirika la Anga (TCAA) akifuatiwa na SUMATRA na EWURA.
Kundi la Maji; Iringa Urban Water Supply mshindi akifuatiwa na Tanga Urban Water Supply.
Kundi la Serikali za mItaa; Hannag mshindi akifuatiwa na Ilala na Misenyi.
Kundi la Hifadhi za Jamii; PPF washindi wakifuatiwa na NSSF, LAPF.
Kundi la Universities; Chuo cha Sayansi ya Afya cha Roman Catholic cha CUHAS mshindi akifuatiwa na Ardhi.
No comments:
Post a Comment