Shaw alichezewa rafu mbaya na Hector Moreno katika eneo la hatari wakati beki huyo akijaribu kufunga katika mechi ambayo United ililala kwa mabao 2-1.
Shaw alitibiwa kwa dakika 10 uwanjani huku akiwa amewekewa kifaa cha kupumulia cha oksijeni kabla ya kukimbizwa hospitali ambapo alitibiwa haraka ili kupunguza maumivu kabla hajasafirishwa kurejea Manchester kwa matibabu zaidi.
Mwamuzi wa mchezo huo hakumuadhibu Moreno jambo lililomkera kocha Luis van Gaal na kitendo cha UEFA kumtangaza Moreno kama mchezaji bora wa mechi ndiyo kimeongeza hasira kwa kocha huyo Mdachi.
Memphis Depay aliifunga timu yake ya zamani dakika ya kabla ya Moreno kupiga kichwa kilichomgonga Daley Blind na kuzama wavuni kabla ya mapumziko.
Narsingh aliifungia PSV bao la ushindi katika kipindi cha pili na kuongeza maumivu kwenye benchi la United baada ya mkasa wa Shaw.
Nchini Hispania Real Madrid iliialika Shaktar Donetsk katika dimba la Santiago Bernabeu kabla ya Ronaldo kuibuka shujaa akifunga magoli matatu na Benzema akimalizia moja kufanya jumla ifike 4-0.
Kwa magoli hayo Ronaldo amemzidi mpinzani wake wa karibu Leonel Messi katika wafungaji wa Ulaya kwa kufikisha goli 80 huku Messi akibakia hatua tatu nyuma.
Mechi hiyo ilishuhudia Sergio Ramos, Gareth Bale na Rafael Varane wakipata majeraha yaliyolazimu kutolewa nje. Rafael Benitez amesema hawajajua rasmi jeraha la Bale litapona huku Ramos akiugulia maumivu ya bega.
Leonel Messi alishindwa kufunga wakati timu yake ikimenyana na AS R oma pale Stadio Olympico katika mechi yake ya100 kwenye michuano hiyo.
Messi anavunja rekodi ya kufikisha mechi hizo kama mchezaji mdogo zaidi kwenye orodha ya wachezaji 33 waliovuka mechi 100 za UEFA.
Luis Suarez alifunga bao la kuongoza kabla ya Florenzi kufunga goli la jabu la umbali wa mita 51.
Matokeo ya mechi zingine ilikua kama ifuatavyo;
No comments:
Post a Comment