Pages

Sunday, September 13, 2015

CRISTIANO RONALDO AVUNJA REKODI NYINGINE


Ronaldo amefikisha jumla ya magoli 230 na kumpiku gwiji wa Real Madrid, Raul aliebakiaa nafasi ya pili akiwa na jumla ya magoli 228.
Imemchukua Ronaldo mechi 203 tu kufikisha goli 230 toka ajiunge na mimba hiyo mwaka 2009 akitokea Manchester United.
Ronaldo alikua katika kiwango cha juu wakati Real Madrid ilipoishindilia Espanyol goli 6-0 katika uwanja wake wa nyumbani huku wakishuhudia Ronaldo akifunga magoli matano peke yake na KarimBenzema kumalizia karamu hiyo.
Maswali yalianza kuzuka juu ya uwezo wake baada ya kucheza mechi mbili za ufunguzi bila kufumania nyavu lakini juhudi zake kwa siku moja zimefuta kumbukumbu zote za ukame wa mabao toka msimu uanze.
Ilimchukua Ronaldo dakika 20 tu kufunga hat trick kabla ya kumalizia mengine mawili katika kipindi cha pili, jambo lililopelekea kumpindua Raul kwenye nafasi hiyo huku akiwa hatua chache kuipindua rekodi ya Raul katika michuano yote. Raul sasa na goli 323 na Ronaldo yuko hatua tanop nyuma jambo ambalo litatokea hivi karibuni kulingana na makali ya Mrebno huyo kwa sasa.
Ronaldo amekua na rekodi nzuri ya ufungaji na takwimu zinaonyesha goli zake zote 318 katika michuano yote zimekuja katika mechi 303 tu ukilinganmisha Raul aliehitaji mechi 741 kufikisha goli 323 tu.
 

No comments:

Post a Comment