Chifu Yemba ni nani?
Chifu Yemba ambaye
ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma, alizaliwa Mbinga mkoani Ruvuma mwaka 1966.
Alisoma shule ya msingi ya Kaluta kati ya mwaka 1975 na 1981.
Alisoma shule
za sekondari za Uyui na Ujiji kati ya mwaka 1982 na 1985. Mwaka 1986 hadi 1987
alisoma kidato cha tano na cha sita katika shule ya Sekondari ya Iyunga mkoani
Mbeya.
Kati ya mwaka
1988 hadi 1990 alisoma katika Chuo Kikuu cha Southern Carolina na kutunukiwa shahada
ya elimu ya viumbe.
Mwaka 1998
alisoma katika Chuo Kikuu cha Frankfurt, Ujerumani na kupata Shahada ya Uzamili
ya Hydrogas. Kisiasa aliwahi kuwa mwanachama wa CUF kabla
hajahamia katika ADC.
Aliwahi kufanya
kazi katika halmashauri ya Kigoma, Ujiji kati ya mwaka 1987 hadi 1997.Hivi sasa
ni mjasiriamali anayejishughulisha na uchimbaji wa madini.
No comments:
Post a Comment