Edward Lowassa mgombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chadema |
Mgombea uraisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia
chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), pamoja na muunganiko wa vyama
vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi
(UKAWA), Edward Ngoyai Lowassa amesafishwa na wanasheria pamoja na wachambuzi
mbalimbali wa siasa hapa nchini.
Wakihojiwa na kituo kimoja cha habari cha Ujerumani cha
radio DOTCH VERE, kuhusu mstakabali wa
Edward Lowassa kujiunga na UKAWA. kila mmoja alionesha kuwa Edward Lowassa yuko
upande sahihi na hajakosea kwa kuzingatia kauli mbiu yake ya “safari ya
matumaini”, na kwamba haiwezi
kupatikana ndani ya chama cha Mapinduzi ila kupitia ukawa. Ifahamike kuwa
Edward Lowassa amejiunga na chadema na kukubaliwa kuchukua fomu ya kuwania
nafasi ndani ya ukawa ili aweze kuchaguliwa na wananchi kuwa Raisi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, baada ya jina lake kukatwa katika mchujo uliofanyika
huko Dodoma kwa chama chake cha awali cha Mapinduzi. (CCM).
Mdau wa kwanza ni Tundu lisu, mbunge wa jimbo la Singida
Mashariki na ni mwanasheria mkuu wa chadema, amemzungumzia Edward Lowassa
Katika sakata la RICHMOND kuwa alishiriki kama waziri mkuu na alichukua uamuzi
wa kujiuzulu kutokana na nafasi aliyokuwa nayo wakati huo, Na yeye kwa
kutambua
hilo aliamua kuwajibika kisiasa kwa kuchukua uamuzi wa kujiuzuru wadhifa wake.Tundu Lissu Mwanasheria mkuu wa CHADEMA(Katikati) |
Hata hivyo ameongeza kuwa, ndani ya chadema hakuna na
hakutakuwa na mpasuko wowote kwani Edward Lowassa hajaokotwa tu jana au juzi ni
muda mrefu wa miezi mitatu iliyopita mpaka wakafikia muafaka kuwa akubaliwe
katika chama. Makubaliano hayo yalifanywa na viongozi wote wa chama wakuu ambao
ni Mwenyekiti, katibu mkuu wa chama, na
viongozi wengine wa chama.
Mdau mwingine aliyechangia ni Yusuf Kamoti ambaye ni
mchambuzi wa siasa amesema, “uchaguzi wowote, katika nchi yoyote, katika jamii
ya watu wowote unapotokea ni jambo la jaribio kwa wanadamu wanaoishi katika
eneo husika” amesema hivyo kwa sababu mgombea ambae anatarajiwa kupitishwa na
Ukawa ni Edward Lowassa na hili ni jaribio kwa wananchi wa Tanzania.
Mwakilishi wa jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jusa |
Alipotangaza nia ya kugombania kiti cha uraisi jijini Arusha
kupitia chama cha Mapinduzi alizitaja agenda ambazo zinafanana kabisa na agenda
za ukawa ambazo ni kufufua uchumi, kupambana na ufisadi pamoja na rushwa,
kuongeza ajira kwa vijana na kutumia rasilimali za nchi kwa manufaa ya wananchi
wote wa Tanzania, hizo ni baadhi tu ya agenda za Lowassa na ndizo zinazofanana
na Agenda za UKAWA, pia katika suala la katiba mpya atazingatia maoni ya
Wananchi na sio maoni ya watu wachache, hivyo ndivyo Ismaail Jussa
alivyomzungumzia Edward Lowassa.
wafuasi wa Edward Lowassa, kauli mbiu yao ni "popote tupo" |
Mdau wa mwisho kuchangia mada ni Aguta Mussa, ni mchambuzi
wa siasa nchini Tanzania, kwa upande wake alisema, kitendo cha Edwarrd Lowassa
kujiunga na upinzani ni tofauti na kitendo alichokifanya Augustino
Lyatonga Mrema ambaye alihama Chama cha
Mapinduzi na kujiunga na chama cha NCCR-Mageuzi akitegemea kupata kiti cha
uraisi kupitia upinzani, lakini haikuwezekana. Utofauti mkubwa uliopo kati ya
hawa wawili ni kwamba Edward Lowassa kajiunga na ukawa wakati tayari ukawa
walikuwa wamekwishakubaliana kujiunga
pamoja na kumpata mgombea mmoja wa uraisi, hivyo kuja kwa Edward Lowassa
kunaongeza nguvu kubwa ya wananchi ambao walikuwa wanapenda Lowassa kuwa raisi
kupitia CCM, na kwa bahati mbaya hakupitishwa. Hivyo watu walewale wa CCM wako
na watakuwa tayari kumchagua Edward Lowassa kuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania hata kama yuko upande wa UKAWA.
Mwisho wa siku ni hapo Oktoba 25 mwaka huu ambapo wananchi
watachukua uamuzi wa kumchagua raisi mmojawapo kati ya Edward Lowassa, John
Magufuli na wagombea wengine kutoka katika vyama vingine vya upinzani.
No comments:
Post a Comment