Msimu wa ligi kuu za soka katika mataifa mbalimbali zinatarajiwa kuanza hapo kesho, macho na masikio ya wapenda soka ni kuitazama ligi kuu ya Uingereza barclays premier league.
kuna timu ambazo zimefanya usajili mkubwa na kuna timu ambazo zimefanya usajili wa kawaida, zote zikiwa na lengo la kutwaa taji la ligi na mataji mengine madogo madogo.
Mechu ya mapema kabisa kwa kesho tarehe 08/08/2015 ni kati ya mashetani wekundu wa jiji la Manchester (manchester United) dhidi ya Totenham hotspurs ambayo itakuwa majira ya saa 8: 45 mchana kwa saa za Afrika ya Mashariki.
Nyingine kubwa ni kati ya Chelesea dhidi ya Swansea city majira ya saa 1:30 usiku kwa saa za Afrika ya Mashariki, ikumbukwe kuwa Chelsea ni mabingwa watetezi wa taji hilo la Uingereza.
kuanzia siku ya kesho wadau wa soka wataanza kufuatilia mwenendo mzima wa ligi kuu ya Uingereza na mataifa mengine hasa kwa upande wa usajili wao, ambapo kila timu ilisajili kadiri ya maitaji yake.
Timu ya Manchester United imewasajili wachezaji watano (5) ambao ni shneiderlin kutoka Southampton, Schweinsteiger kutoka Bayer munichen, Matteo Darmian kutoka Torino nchini Italia, na Sergio Romelo aliemaliza mkataba wake na klabu ya Sampdoria, ya nchini Italia.
Pia klabu ya Chelsea imesajili wachezaji watatu kwa msimu hu ambao ni Radamel Falcao, kwa mkopo kutoka klabu ya Monaco, Asmir Begovic kutokea Stock city pamoja na Kenedy akitokea Brazil, na amekwenda kwa mkopo klabu ya Vittese.
Kwa upande timu ya Arsenal mpaka muda huu wamemsajili Per Cech kutokea klabu ya Chelsea, kutokana na kuimarika kwa kikosi cha klabu hiyo wanaona hakuna haja ya kuongeza wachezaji wengine wapya, kwani katika mechi za mwisho za ligi iliyopita walifanya vizuri sana na kwa kipindi cha mechi za majaribio pia walifanya vizuri kwa kuychukua mataji matatu .
Swali linakuja, timu gani inayopewa nafasi ya kutwaa ubingwa mnsimu huu? kutoka na usajili uliofanyika na nguvu ya kikosi.
No comments:
Post a Comment