Pages

Saturday, August 8, 2015

REKODI ZA SIKU YA JUMAMOSI KATIKA LIGI ZA ULAYA



Juventus imenyakua ubingwa wa CoppaItaliana kwa mara ya saba leo, mara nyingi zaidi.
Giainluigi Buffon amevunja rekodi ya ushindi zaidi kwenye SuperCoppa Italia, mara 6 akimzidi Dejan Stankovic.
Kocha wa Juventus Maxi Allegri anaingia kwenye list yaa makocha walioshinda CopaItalia na klabu mbili tofauti baada ya Fabio Capello na Rafa Benitez.
Mario Mandzukic ameshinda mechi za Supepr Cup katika nchi tatu tofauti akifanya hivyo Ujerumani, Spain na Italia.Kila mechi ya Super Cup aliofunga bao Mandzukic timu yake iliibuka na ushindi.
Hii ni mara ya kwanza kwa mechi ya ufunguzi wa Barclays Premier league kuwa na goli la kwanza la kujifunga.(Kyle Walker, Tottenham vs Manchester United)
Hii ni mara ya pili kwa Spurs kujifunga kwenye mechi ya ufunguzi dhidi ya United, ya kwanza mwaka 1997.
Manchester United wamepata clean sheet kwa mara ya kwanza ya ufunguzi toka mwaka 2010 walipoifunga Newcastle 3-0.
Maanchester United sasa wameshinda mechi 24 za ufunguzi zilizzochezwa Old Trafford, ikidroo mara 6 na kupoteza moja tu.
Everton wamepata droo ya 2-2 katika mechi ya ufunguzi kwa mara ya tatu mfululizo.
Everton sasa wameruhusu magoli 37 kwenye mechi za ufunguzi, zaidi ya timu zingine zote EPL.
Jermaine Defoe sasa aamefunga katikaa misimu 15 ya ligi kuu England akifikisha jumla ya goli 129 leo.
Ni Batefimbi Gomis na Nailsmith Steve pekee waliozifunga Arsenal, Chelsea, Manchester City na Manchester United kwa muda wa mis mu miwili ya ligi kuu England.
Swansea ni timu ya kwanza kufunga magoli mawili Stamford Bridge baada ya kufanya hivyo mwaka jana September.
Kadi nyekundu ya Courtois ilikua ya 70 kwa Chelsea, kadi 17 zimetoka katika utawala wa Mourinho. (24%)
Oscar amefunga maagoli matatu katika michezo 12 iliopita, yote dhidi ya Swansea City.

No comments:

Post a Comment