Nicolas Otamendi baada ya kusainishwa Etihad leo mchana. |
Manchester United imepata pigo lingine baada ya mchezaji Nicolas Otamendi kusajiliwa na mahasimu wao wakubwa Manchester City. Otamendi aliehusishwa na kujiunga United kwa muda mrefu amesaiani mkataba wa miaka mitano baada ya kusajiliwa kutoka Valencia kwa dau la Euro mil 45.
Otamendi ataungana na rafiki yake waliecheza nae huko Portugal, Eliaqium Mangala aliesajiliwa Etihad msimu uliopita kwa ajili ya kuongeza makali ya ulinzi wa Man City. Kwa United hii ni habari mbaya baada ya kushindwa kuwasajili Sergio Ramos alieamua kubaki Santiago Bernabeu, Perdo alieko mbioni kujiunga Chelsea na sasa Otamendi aliejiunga kwa mahasimu wao wakubwa City.
No comments:
Post a Comment