Pages

Thursday, August 20, 2015

UNITED WAMGEUKIA SADIO MANE BAADA YA KUMKOSA PEDRO




Akiwa amefunga magoli 10 katika mechi 32, Mane amegeuka kuwa mbadala wa winga anaehitajika kutua Old Trafford kabla dirisha la usajili halijafungwa. Van Gaal amehamishia macho yake kwa mchezaji huyo mwenye miaka 23 alieko St Marrys.
United waliokua wanahusishwa kwa nafasi kubwa kumsajili winga wa Barcelona Pedro walijitoa kwenye meza ya mazungumzo huku wapinzani wao wa ligi kuu ya Englamd Chelsea wakimtwaa kwa dau la mil 30. Van Gaal anaona Mane bdio mbadala wa Angel di Maria alietimkia PSG hivi karibuni. 
SAIDO MANE vs UNITED STRIKING FORCE 2014-15
Sadio  Mane anashikilia rekodi ya hat trick ya mapema zaidi kwenye ligi kuu ya Uingereza baada ya kuifunga Aston Villa ndani ya dakika 2 na sekunde 55 msimu uliopita 2014-15. 
Katika msimu uliopita ni Wayne Rooney (12)pekee aliefunga magoli mengi kuliko Mane (10).
Southamptom wamekiri kuwa United imeonyesha nia ya kumsajili na haiko tayari kupoteza mchezaji mwingine wa 3 muhimu kwenda Old Traford   ndani ya mwaka mmoja baada ya kuomdoka kwa Morgan Schneiderlin na Like Shaw. 
SOURCES; Goal.com/en na Opta Stats

No comments:

Post a Comment