PreudeHomme akiondoka uwanjani Old Traford na msaidizi wake juzi usiku |
Kocha wa timu ya Club Brugge Michel Preud'homme amekiri kuwa timu yake ina nafasi ndogo sana ya kufuzu hatua ya makundi ya Uefa Champions league kufuatia matokeo ya 3-1 waliyopata katika mchezo wa kwanza pale Old Trafford.
Club Brugge walipata bao la kushtukiza dakika ya 8 baada ya kiungo Michael Carrick kujifunga akijaribu kuokoa mpira wa adhabu uliopigwa kuelekea langoni kwao. Dakika chache baadae usajili mpya Memphis Depay aliwachambua kwa umakini mabeki wa Brugge kabla ya kuachia shuti langoni kwao lililomshinda mlinda mlango wao. Depay ambae ameshindwa kupata bao katika mechi mbili za awali dhidi ya Tottenham na Aston Villa alikua kwenye form baada ya kuongeza bao la pili kabla ya Marouane Fellaini kumalizia la tatu dakika ya mwsiho ya mchezo jambo lililopekea kocha huyo kuona hawana nafasi ya kuwafunga mechi ya marudiano nyumbani kwao Ubelgiji.
Michel anaona kikosi chakle kina kibarua kigumu katika mechi ya marudiano ukizingatia hatokua na huduma ya captain wake Mechele ambae alipata kadi nyekundu huku wimbi la majeruhi likiiandama timu hiyo hivyo kuona ana nafasi ndogo sana ya kuifunga United ambayo ilitawala sehemu kubwa ya mchezo wa awali pale Old Trafford.

No comments:
Post a Comment