Wakati mbio za uchaguzi
mkuu wa uraisi, ubunge na udiwani zikipamba
moto katika kila kona ya nchi, wagombea na wafuasi wao wakijigamba
kushinda kwa kishindo katika uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo Oktoba 25,2015.
mgombea uraisi kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Edward Ngoyai Lowassa akiwa na mkewe Bi. Regina Lowassa mara tu walipokabidhiwa kadi za chama |
John Pombe Magufuli ni
mgombea wa uraisi kupitia Chama cha Mapinduzi
(CCM) anatarajia kupata upinzani mkubwa
kutoka katika vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) ambavyo ni CHADEMA, CUF, NCCR-MAGEUZI na NLD.
Kwa upande wa chama cha
Mapinduzi kesho tarehe 01/08/2015 ndiyo siku ya kuchaguliwa wabunge wao
waliotangaza nia ya kugombea ubunge kwa majimbo husika. Kwa lugha nyingine
tunaweza kusema kwamba, kesho ni siku pekee ya kukatwa kwa baadhi ya
waliotangaza nia na wachache wao
kupitishwa.
mgombea uraisi kupitia chama cha demokrasia na maendeleo, Edward Ngoyai Lowassa akisisitiza jambo kuwa ana imani na ukawa pia ana imani na ushindi hapo Oktoba 25 mwaka huu. |
Kwa upande wa ukawa
wamekwisha gawana majimbo mbalimbali kwa kuzingatia chama gani kinakubalika
mahali gani. Lowassa pamoja na Ibrahim
Lipumba ni wagombea pekee kwa upande wa ukawa, mmoja wao atapata nafasi ya kupeperusha
bendera ya umoja huo.
Hawa ni baadhi ya watu wanaojiita team Lowassa popote aendapo nao wapo, anaonekana msichana shupavu Christina Mshiu ambae ni msomi wa chuo kikuu. |
No comments:
Post a Comment