Pages

Friday, August 28, 2015

MESSI BORA ULAYA



Mshambuliaji wa timun ya Barcelona Leonel Messi amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya akiwagaragaza Cristiano Ronaldo wa Real Madrid na mwenzake wa Barcelona, Luis Suarez.
Messi ametwaa tuzo hiyo kufuatia msimu mzuri wa 2013-14 ambapo aliisaidia klabu yake kubeba ubingwa wa Hispania, Kombe la Mfalme na Klabu Bingwa ya Ulaya.
Messi alifunga jumla ya mabao 67 katika mechi 62 alizocheza kwa klabu na timu ya taifa msimu uliopita hii ikimaanisha atavutana tena na Cristiano Ronaldo katika tuzo za Mchezaji Bora wa Mwaka hapo January mwakani. Messi alichukua tuzo hiyo kwa mara ya kwanza mwaka 2011 baada ya kuisaidia BARCELONA Kkuoata ubingwa wa Ulaya.
Tuzo hiyo ilitolewa jana jioni wakati wa upangaji wa makundi ya klabu bingwa ulaya kwa ajili ya msimu wa 2015-16.

No comments:

Post a Comment